Showing posts with label Uncle Jimmy. Show all posts
Showing posts with label Uncle Jimmy. Show all posts

Thursday, June 7, 2012

EXCLUSIVE ENTERVEW - JOHN LISU

Yapo Mambo Mengi ambayo unatamani kuyajua kupitia Muimbaji wa Mziki wa Injili anaefanya vizuri Tanzania,Kenya,Rwanda na Uganda si mwingine ni John Lisu.Siku ya leo amepiga Story na Blog kuhusu maisha yake ya Muziki familia na kauli aliyoitoa Muimbaji Stara Thomas siku chache zilizopita.

Kama kawaida majira ya asubuhi nafika Nyumbani kwa John Lisu nakuanza mahojiano naye.Kabla ya yote nilitaka kujua nini ambacho kilimpeleka Kenya.Unataka Kujua gonga hapa??

Exclusive Uncle Jimmy No 1


Sikuishia hapo nikamuuliza analipi lakusema juu ya Kauli ya Muimbaji Stara Thomas kwa kauli yake ya Waimbaji wa mziki wa Injili hawana Upendo,Ushirikiano na Wanafki.

Exclusive Uncle Jimmy No 2


Nilimuliza pia yapi mafanikio aliyo yapata kwa kazi yake ya Muziki wa Injili aliyoifanya kwa Muda mrefu.

Exclusive Uncle Jimmy No 3


Sifa ya John Lisu popote anapokuwa jukwaani utumia Gita kama kitambulisho kinacho muonyesha yeye nimwanamuziki alie kamilika katika uimbaji.Nikataka kufaham je,mziki wake umepenya katika mipaka ya East nikimanisha Kenya,Uganda na Rwanda.

Exclusive Uncle Jimmy No 4


John ni mtu ambae upenda kucheka sana na mara nyingi usema anapenda kufurahi na hasa kucheka.Lakini ziko tabia ambazo hazipendi hasilani katika Maisha yake.Gonga hapa twende sawa.

Exclusive Uncle Jimmy No 5


John kama leo ingetokea Sheria yakukuzuia wewe kuimba ungefanya kazi gani kwa mfano.

Exclusive Uncle Jimmy No 6


Kila Mtu katika Maisha yake analo jambo ambalo hawezi kusahau iwe kupitia jaribu au kupitia kitu flani kilicho mtokea.Kitu ambacho John hawezi kusahau ni pale Malaika alipomtokea nakuongea nae.Sio kumtokea ndotoni kama wengi wasemavyo bali kwa macho ya Nyama.Sikia maneno yake.

Exclusive Uncle Jimmy No 7


Kwa sasa John Lisu anafurahia Maisha ya Ndoa yake yenye Mwaka mmoja Nanusu toka kufunga Ndoa.Pia Mungu amempatia Mke mwenye uwezo wakupiga Gita kama afanyavyo yeye japo mkewake sio muimbaji.

Pata Video Exclusive Mke wa John akicheza na Gita.


Biblia aikukosea kusema Mungu ukupa wakufanana nawe nimeamini kupitia Familia hii yenye furaha na amani katika Maisha ya Ndoa yao.Nae John Lisu akuacha kunishangaza kwakunipa ladha ya wimbo alio urecord siku 3 nyuma.

Exclusive Uncle Jimmy.


PICHA NANE NIKIWA NYUMBANI KWA JOHN.
Kifa Cha Kazi
John Lisu na Mkewe Nelly.

Peopleeeeee.
Hii ni Tuzo aliyoshinda Mwaka 2010 ya Video Bora ya Mwaka.
Atuvumi lakini tumo.Nikionyesha uwezo wangu enzi hizooooooooo FGBF.








Wednesday, June 6, 2012

KAMA WEWE NI DJ NAUNA KIPAJI HII INAKUHUSU.

Radio Praise Power Fm 99:2 inakutafuta wewe Dj mwenye uwezo wakufanya Mixing nzuri na Utundu katika kucheza na Mashine ya Dj.Kama unakipaji basi nisehemu yako kuonyesha uwezo uliokuwa nao kupitia Radio ya Faraja Praise Power Fm.

Shindano hili lakutafuta DJ mkali linasimamiwa na Praise Power kupitia kipindi kinacho fanya vizuri cha Sifa Moto.

VIGEZO
1}Uwe umeokoka
2}Usiwe chini ya umri 18
3}Wahi kuchukua fomu yako Praise Power fm
4}Sikiliza Sifa Moto ilikujua kama jina lako litapita katia shindano
5}Ukisha chukua fomu yako ya ushiriki unaitajika kuwai saa moja kabla yakipindi cha Sifa Moto kuanza.

Shindano hili la Dj litachukua Mwezi mmoja na baada ya hapo kutakuwa na Fainali zitakazo fanyika Sinza Africar Sana kwenye Shule ya Kenton.

Kwa maelezo zaidi Gonga hapa twende sawa.


Pata Video ya Maojiano yangu na George Mpela juu ya Shindano hili.


Pia unaweza kuhuliza Chochote iwe swali au wataka kujua zaidi,Tumia namba zifatazo.
Dj Erick Brighton wa Ppr Fm-0715-408566
Uncle Jimmy-0774-763939.
Ukitaka kufika Ofisi zilizopo Radio Praise Power,ni Mikocheni B katika kanisa la Mlima wa Moto.







STARA THOMAS AWAJIA JUU WAIMBAJI WA GOSPLE.

Siku ya jana katika kipindi cha Sifa Moto kinachoongozwa na George Mpela na Nice Noel kimezua mjadala mkubwa baada ya Muimbaji aliyekuwa akiimba Bongo Freva Stara Thomas kuwajia juu waimbaji wa Mziki wa Gospel,nakusema wengiwaho awana Upendo,Wanafki,awana ushirikiano.
George Mpela na Nice Noel.

Bibie Stara Thomas baada yakupokea wokovu amekuwa akiomba mchango wa Mawazo kwa waimbaji wenzake ilikuweza kuifanya kazi ya mziki wainjili vizuri,matokeo yake anakutana na waimbaji wenye roho ya Uchoyo,Umimi,Ubinafsi na kukatishwa tamaa.

Katika Albam aliyoipa jina "Nani ni Mshamba'anasema muimbaji aliyekubali kufanya nae kolabo ni mmoja tu Faraja Ntaboba ambae anatokea Kongo.Alijaribu kuwafata waimbaji wengine ilikumpa msaada katika toleo lake wakamchinjia baharini.Wengi waho aliowafata walionekana wapotayari kumsaidia kwa Macho,lakini katika vilingi vya moyo awapo tayari.
Nice Noel.

Nisikuchoshe kwa Maneno mengi sikiliza Maojihano yake na Kipindi cha Sifa Moto jana.
Gonga hapa twende sawa.


Wakati Stara Thomas akifunguka huko George Mpela na Nice Noel wakataka kujua likowapi tatizo kwa waimbaji wa Mziki wa Injili mpaka kufikia hatua ya Stara Thomas kufunguka kiasi hicho.

Wakamtafuta Muimbaji John Shabani ilikutaka kujua ayasemayo Stara Thomas nikweli nakama nikweli yapo.
Gonga hapa twende sawa.


Niukweli usio pingika waimbaji wa Mziki wa injili wamekuwa awapendani,waho kwa waho wanachukiana pasipo sababu yoyote.Je?Kwa hali hii tunakwenda wapi.Kama Mungu anamleta Kondo nyikani alafu sisi tunamtenga nisawa.Jibu unalo

Kwa maoni au Ushauri,Tuma kupitia Namba hii hapa yatawafikia George na Nice 0774-763939

Saturday, June 2, 2012

KUFIKA UMRI HUU 84 NI NEEMA.HAPPY BIRTHDAY BISHOP DR.MOSES KULOLA.

Moses Kulola.

Bishop Dr.Moses kulola leo ametimiza Miaka 84 toka kuzaliwa kwake.Mungu akupe maisha marefu naazidi kukutimia kilaitwapo leo.Blog inakutakia sherehe njema ukiwa na Familia yako apo Mwanza.

Haya ndio yaliyojiri katika Happy Birthday ya Moses Kulola.
Mpakwa mafuta wa Bwana Bishop Moses Kulola akikata Keki.
Moses Kulola akimlisha Keki mkewe,kwa eshima ya Mume wake Mama alipiga magoti.
Mama hakuwa nyuma kumlisha Keki mumewe.
Mtoto wa Moses Kulola,Daniel ambae ni Mchungaji akilishwa Keki.
Masanja Mkandamizaji nae alikuwepo katika tukio zima la Keki.








CHRISTINA SHUSHO KWA MARA NYINGINE TENA 2012 NDANI YA TUZO ZA "AFRICA GOSPLE MUSIC AWARDS"

Yakiwa majira ya Saa 4:00 jioni napata taharifa muimbaji Christina Shusho ameingia kwenye kinyang"nyiro cha Tuzo za Africa Gosple Music Awards.Nami bilakupoteza Muda nikamtafuta Christina Shusho kwenye Simu yake ya Mkononi 0715-6677........alikuwa na haya yakusema.
EXCLUSIVE ON UNCLE JIMMY.


Hatimaye kamati inayoandaa tuzo za Muziki wa Injili barani afrika siku ya jana imetoa orodha ya wanamuziki ambao watakuwa wakichuana katika kutafuta washindi wa Kategori mbalimbali.Kwa mujibu wa kamati hiyo mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Mwanamama Christina Shusho amefanikiwa kuwa mwanamuziki pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuingia katika tuzo hizo mwaka huu na ameibuka katika kategori mbili ambazo ni Mwamamuziki bora wa Afrika Mashariki pamoja na mwanamuzik bora wa Kike Barani Afrika.



Christina Shusho amekuwa rafiki yangu wakaribu sana,ukiacha kuchaguliwa uko ni mtu anaekubali kupokea mawazo mbalimbali ya watu.Ivyo Mwaka jana nilimshauri kujaribu kufanya Video zake na watu wa Mataifa japo najuwa kwa hili wengi mtanipinga ila niukweli usiopingika baadhi ya Video za waimbaji wa Mziki wa Injili ni kichefuchefu kuziangalia.
John Kalage na Christina Shusho.

Kupitia Albamu yake ya Nipe Macho Nione nilimpeleka kwa kijana JOHN KALAGE ilikuweza kupata picha nzuri na ubunifu mwingine wakuanzia Mavazi adi sehemu zakufanyia Shooting.
Nikiwa na Christina Shusho ofisini kwa John Kalage Mwaka jana Mwezi wa Tatu.

VIPENGELE ANAVYO WANIA.
1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria

1.Eko Dydda- Kenya
2.Emmy Kosgei - Kenya
3.Exodus- Uganda
4.Christina Shusho- Tanzania
5.Lam Lungwar- South Sudan
6. Sarah K- Kenya
7.Dawit Getachew-Ethiopia
8.Kambua-Kenya
9.Willie Paul- Kenya
10.Ann Marie Mutesi - Burundi

Ilikuweza kumpigia kura Christina Shusho nakuibuka mshindi katika Vipengele hivi viwili.Ingia kwenye Tovuti hii {http://www.africagospelawards.com/nominate.html}
VOTE NOW
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.




MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 2009.

Leo katika Hotel ya Wanyama iliyoko Sinza yalitolewa Mafunzi kwa Waandishi wa Habari juu ya Sheria mpya ya Mtoto ya Mwaka 2009.Gloria Mafole kutoka kituo cha Sheria na Haki za bainadamu {LHRC}alieleza wajibu wakila Mtanzania kujua sheria mpya ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Wakili Gloria Mafole akieleza nini Sheria ya Mtoto.


SHERIA YA MTOTO INAHUSU NINI?

Sheria hii ya Mtoto inazungumzia:
a}Sheria za Mtoto,
b}Haki za Mtoto,
c}Kukuza,Kulinda na Kuhifadhi ustawi wa Mtoto,
d}Masharti ya unasibishaji wa Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa,
e}Maswala ya kulea,kuasili na uangalizi.
Pia inatoa maelezo na masharti yanayohusu mtoto anapokuwa katika migogoro na Sheria.
Waandishi wa Vituo mbalimbali vya Habari wakifatilia Mafunzo na Mjadala wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Mr Mnubi akifatila kwa makini mjadala.
Kama Kawa nikiwakilisha Praise Power Fm.

HAKI NA USTAWI WA MTOTO.

Mtoto ni nini?
Mtoto ni mtu aliye na umri chini ya miaka kumi na nane.Zipo haki nyingi katiaka kifungu 158 cha 2009 kinacho onyesha Haki na Ustawi wa Mtoto.Kifungu hiki kimeweka bayana hairusiwi kuonyesha Picha zozote mbaya mf:-Watoto waliobakwa,Mtoto aliekeketwa,Mtoto aliechomwa moto kisa kaiba shilingi 200.
Dr Jeremia Makuli Mratibu wa mradi shirika la CDIP akichambua jambo.

Kifungu No 11 Mtoto anahaki yakutoa Mawazo,Kifungu No 8 kinaeleza wajibu wa wazazi kuwapa watoto Elimu,kucheza na kupumzika,Wajibu wakuwapatia Mavazi,Kuwalinda na Vitendo vya ukatili.

Mafunzo haya ya Haki za Mtoto yameandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali CDIP {COMMUNITY DEVELOPMENT INITIATIVE PROFESSIONALS},liliopo Tegeta Kibaoni linalo jishughulisha na Maswala ya jamii.
Wafanyakazi wa CDIP
Joyce Josepht -Mratibu CDIP.
Dr Ritha Mutayoba-Mratibu CDIP
Vyombo vya Habari vikiwa Busy kuakikisha jamii inalipata tukiozima.





Friday, June 1, 2012

JICHO LA BLOG na MASANJA MKANDAMIZAJI.

Wengi mnamjua kama mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi "Masanja Mkandamizaji"Lakini kupitia Jicho la Blog Masanja ni Muimbaji na sasa ana Albamu inayokwenda kwajina la "HAKUNA JIPYA"ambapo ndani ya Albamu yake zipo Nyimbo 10 alizo record Studio tofauti tofauti.

Sikiliza song moja katika Albamu yake iliyojaa vichekesho na burudani.'Hakuna Jipya"




PIPOOO!! ALBAMU YA MASANJA MKANDAMIZAJI
Muonekano wa Kava ya Albamu ya Masanja a.k.a Pastor Mtarajiwa.


















Thursday, May 31, 2012

Mchungaji na Mtangazaji Harris Kapiga "Kuteta" ndani ya Women in Balance.

Mchungaji na Mtangazaji wa clouds Fm Harris Kapiga anatarajiwa kuwa Msemaji katika Women in Balance.Akiongea na Blog hii alikuwa na haya yakusema.

Harris Kapiga-Nimeitwa kwenda kutoa somo ni jinsi gani mwanamke alinde ndoa yake isiingie na Mikwaruzo/Kama ipo afanyaje ilikuokoa Ndoa yake.Naamini kupitia uzoefu niliokuwa nao katika ndoa naweza kuwasaidia Mabinti waleo wanaotamani kuolewa.Zipo Changamoto nyingi katika Ndoa ivyo kupitia Women in Balance naimani itakuwa msaada kwao.Mwisho wakunuku.
Hariss Kapiga.Motivational speaker

Kwa mujibu Harris Kapiga event hiyo itakuwa Tarehe 9/june 2012 majira ya 7 mchana mpaka Saa 1 usiku



















Wednesday, May 30, 2012

MKUTANO WA INJILI DAR ES SALAAM VIWANJA VYA BIAFRA KINONDONI.

Tuesday, May 29, 2012

MUIMBAJI WA GOSPEL THAMI MAGWAZA WA AFRIKA YA KUSINI AFARIKI DUNIA.

Huzuni Kubwa imetanda Nchini Afrika ya Kusini kupitia Kifo cha Muimbaji wa Kundi la Spirit of Praise "Thami Magwaza".Thami amefariki dunia siku ya Jana asubuhi baada ya kukimbizwa Hospitali akiwa amepatwa na Mafua ya ghafla.Akiwa katika matibabu ya haraka ilikuokoa maisha yake,ndipo Mauti ilipo mfika.
Marehemu enzi ya Uhai wake.
Thami Magwaza.

Hakika atakumbukwa kwa Mengi kupitia kipawa alichokuwa nacho,Thami alishafanya kazi na waimbaji Maarufu Afrika ya Kusini kama,Pastor Benjamin Dube, Solly Mahlangu,Keke Phoofolo, Zanele na wengine wengi.


Pata Video ya Marehemu akiwa na Kundi la Spirit of Praise enzi ya uhai wake.









Yaliojiri uwekaji Wakfu CD za DsmgospelBand..

Siku ya Tarehe 27/5/2012 Band ya Dsmgospelband waliweka wakfu CD zaho mbili 1}Safari ya Mbinguni,2}Liko Lango.Maombi ya uwekaji wakfu yalifanyika Kanisa la KKKT Tabata Kisukulu.Kwa sasa CD zaho zinapatikana kwa Mkurugenzi wa Band Mr Ahaz kwa Simu namba 0715-71O186
Mchungaji akiweka Wakfu Cd za Dsmgospel Band J/pili ya wiki iliyopita.


Wazee wa Tifua tifua

Kanisa la KKKT Tabata Kisukulu.

Monday, May 28, 2012

HALI SISHWARI ZANZIBAR POLISI WALIPUA MABOMU YA MACHOZI...

Hali ni mbaya Zanzibar kufatia kukamatwa kiongozi wa kikundi cha uamsho.Baadhi ya wafuasi wa kikundi hiko wameamua kuandamana huku jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wafuasi wa kikundi cha uamsho.Hali inaendelea kuwa tete na hivi sasa baadhi ya wafuasi hao wameingia mtaani wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo.

Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed.

Mabomu ya Machozi yakipigwa kuwatawanya waandamanaji.


Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine.
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.
“Sisi wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini, mbona Sudan ya wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao” alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua mikono na kusema ndiooooo.
Awali Sheikh Farid alisema salamu hizo anataka zimfikie Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin moon ambaye kwamba wazanzibari wamechoshwa na kuwepo ndani ya Muungano ambao umedumu kwa miaka 48 lakini bado ukiwa na kero nyingi na malalamiko ambayo yanaonekana utatuzi wake ni mdogo na usiowezekana ambapo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna manufaa yena na wazanzibari.Habari kwa hisani ya zanzibaryetu.wordpress.com








E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP