Monday, November 11, 2013

INAWEZEKANA UZURI WA CHRISTINA SHUSHO NDIO UNAO CHANGIA EVENT YA TAREHE 24/11/2013

By Jimmy  |  8:23 PM No comments

Kati Ya Projects ambazo pia zimenirudisha Mapema Mtaani
ni Hii Kitu Ya Christina Shusho Mwanamuziki wa Injili ambaye mwaka 2013 amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Kutoka Africa Gospel Music Awards.
 Binafsi Christina Shusho ni Maswahiba sana, Miaka kadhaa iliyopita Mimi na swahiba Prosper Alfred Mwakitalima tulienda kupiga kazi Singida tukiwa na Victor Aron... kuanzis siku hiyo tukawa tunaitana "Mtumishi Asiyekuwa na Kipato" tunakumbuka enzi hizo tunapiga kazi hakuna kupeana nauli wala maji ya kunywa tunaambiana "sisi ni watumishi tusio na Kipato".
 
Mwaka 2011 wakati ninapata idea ya kuanzisha wazo la kipindi cha TV ambalo limetimia mwaka 2013. Nakumbuka mwaka 2011 tukiwa Tamal Hotel nilimwita Shusho kwa ajili ya Ku-test interview ya TV ukweli alikuja asubuhi kama saa 3 na sisi tukasema tunafanya kazi kama Watumishi tusio na Kipato nakumbuka nilikuwa na James Temu kama Director, Amani Paul Gaseri kama Cameraman na Editor...tazama kazi yetu mwaka 2011...http://www.youtube.com/watch?v=L6GuCcn1H9k.

Mwaka 2011 ndipo pia tulipata idea ya Friends On Friday-FoF...nakumbuka katika Event ya Kwanza kabisa ya Friends On Friday niliongea na Shusho aje kama kawa Mtumishi asiye na Kipato Shusho akaja tukafanya Collable na Miriam Lukindo Wimbo wa Nipe Macho Nione...tazama hii http://www.youtube.com/watch?v=39wqPZB7k3M.

Mwaka 2012 wakati wa tuzo za Africa Gospel Awards...Shusho akaniomba niende Uingereza kwenda kumuwakilisha katika Tuzo hizo hapo tulikuwa Clouds FM. Sikiliza hiii hapa tukiwa na Harris Kapiga na Victor Nixon...http://www.youtube.com/watch?v=vhZKW2Z9TYw.

Mimi na Shusho hatujakutana barabarani Mwaka 2013 Shusho akaingia tena katika kinyang'anyiro Cha Africa Gospel Music Awards....Kama kawaida kwa Moyo wa Utumishi usio na Kipato Kupitia Chomoza Ya Clouds Tv tukapiga Promo....akafanikiwa Kutwaa Tuzo. Akarudi tukaenda mpaka nyumbani kwake kula Ubwabwa.

Mimi na Shusho hatujakutana barabarani kwani hata tulipompa wazo la Collable na John Lisu kwenye live recording pale CCC Upanga haikuwa ngumu Kiivyoo sababu sisi ni Watumishi tusio na Kipato

Mimi na Shusho hatujakutana barabarani Kwenye harusi yangu ni kati ya wanamuziki wachache wenye majina ambao walitoa support kubwa sana ilikuwa aje sema akaenda katika awards nchini Kenya.


Kikosi kazi kilichofanya Kazi ya John Lisu live recording kikiongozwa na Prosper Mwakitalima...na Prezzor Fredy Chavala-The King na Fred Msungu kimebeba event ya Shusho. Kwa sababu hiyo siwezi lala wakati mtu ambaye hatujakutana barabarani anafanya jambo kubwa namna hii.

Tarehe 24 November, 2013 Kitu Cha Nataka Nikujue Cha Christina Shusho Live Recording...Kitakuwa hewani. Dont Plan to miss this event. Wanamuziki mahiri Samuel Yonah, Amani Kapama, Danny Big-rube Silandah watabeba show nzima hii hapa.

 
Na Blogger Samuel Sasali

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP