Baada yakuwa Kimya kwa Muda mrefu Gospel Star Search yaja kivingine.Mwenyekiti wa Maandalizi Harris Kapiga amefunguka kwenye Blog hii nakusema watu wakae mkao mzuri kuona vipaji vipya vitakavyo ibuka Mwaka huu 2012.
Wakiwa katika Maandalizi ya Shughuli nzima leo waliongea na washiriki walio shiriki Gospel Star Search ya Mwaka 2005 ambapo mshindi wa shindano ilo alikuwa Jessica Honore Kaziri.
Gospel Star Search itakuwa ya utofauti kwani mwaka 2005 aikuweza kuonekana kwa sana kwenye vyombo vya Tv lakini now kupitia Tv ya Clouds itakuletea mchakato mzima kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Maandalizi HK.
Mchakato mzima wa Gospel Star Search utaanza rasmi mwezi April nautachukua miezi mitatu ili kukamilisha zoezi zima nakupatikana mshindi.
0 comments: