Nabii
Samwel Mahela wa Kanisa la Pentecostal Power Ministry (PPM)
lililopo Mikocheni A (katikati mwenye suti), akitoa huduma ya maombezi katika
kanisa hilo.
MSANII wa Filamu aliyejitambulisha kwa jina
moja la Jane amedai amepona ukimwi baada ya kuombewa katika Kanisa la
Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikochezi A.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanila
hilo Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii wakati akitoa ushuhuda wa kupona
ugonjwa huo alisema ana mshukuru mwenyezi mungu na Mchungaji kiongozi wa Kanisa
hilo Nabii Samweli Mahela kwa kumuombea na kupona.
"Nampashukurani zangu mungu kwa
kuniponya kupitia mtumishi wake Nabii Mahela nimeteseka sana na ugonjwa huu
aleluya sasa nimepona"alisema Jane na kushangiliwa na waumini wa kanisa
hilo.
Jane alisema alianza kuugua ugonjwa huu
zaidi ya miaka 10 iliyopita na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali bila
kupata nafuu mpaka alipoambiwa na mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyemtaja
kwa jina la Onesmo kuwa kuna watu wanapona baada ya kuombewa katika kanisa hilo
na Nabii Mahela.
"Baada ya kuambiwa kuhusu uponyaji
huo nilifika kanisani hapa na kuonana na Nabii Mahela ambaye alinifanyia maombi
mfululizo na kuona hali yangu ikibadilika na sasa afya yangu
imeimarika" alisema Jane.
Akizungumza kuhusu suala hilo
Nabii Mahela alisema mbele za mungu hakuna lisilo wezekana kama ilivyowezekana
kwa Jane kwa kuwa aliamini atapona kwa maombi na kweli amepata nafuu jambo la
kumshukuru mungu.
"Biblia inasema kila aaminie
atapona kwa jina la kristo na ndivyo ilivyotokea kwa Jane" alisema
Nabii Mahela.

0 comments: