Mtawa mmoja wa kanisa katoliki
aliyefahamika kwa jina moja la sister Kapuli ameuwawa kwa kupigwa risasi
kichwani na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika eneo la River side
Ubungo jijini Dar es Salaam na kutoweka na pochi ya sister huyo inayodaiwa kuwa
na fedha ambazo
kiasi chake hakikufahmika mara moja.
Sr Kapuli wa
parokea ya Makoka jijini Dar es Salaam ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na
watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi baada ya kufuatiliwa nyendo zao
wakitokea katika benki ya CRDB ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati
akimsubiri Sr Mwenzie aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba
za usajili T 213 CJZ Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani
katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa
waendesha bajaji bw godfrey severine ambaye amenusurkakatika tukio hilo bada ya
bajaji yake kupigwa risasi kadhaa amesema watu hao walifyatua risasi kadhaa
zilizosababisha taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo
kupata upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.
Chazo cha habari matukioblog
0 comments: