HITMISHO LA MSIMU WA KWANZA KATIKA HAZINA YA MAARIFA
(BADILI CHANZO CHA TAARIFA)
Rafiki msomaji wa safu hii ya hazina ya maarifa ni
heshima yangu kubwa sana kukushukuru kwa kunipa nafasi na muda wako ili nikuhudumie kwa njia ya
maandishi.Imekua safari ndefu ya majuma kadhaa ambapo kwa pamoja tulipata wasaa
wa kujifunza juu ya taarifa na namna jinsi ambavyo taarifa inaweza kua ni
chanzo cha matokeo fulani katika maisha yako.Tumejifunza na kuangalia mambo
mengi sana hasa kuhusiana na vyanzo mbali mbali vya taaarifa jinsi vilivyo na
uwezo mkubwa wa kubadili maamuzi yako na tuliona kwamba maamuzi huleta hatua ya
matendo na tendo ndilo huleta matokeo.Sasa watu wengi tumekua tukishugulika
sana na matokeo na kusahau kwamba mzizi wa tatizo au mafanikio si matokeo bali
ni ile taarifa ulioipokea na kuiamini.Hivyo aina ya taarifa unayoipokea itaamua
sana aina ya hatma yako pia,Ninaamini kwa namna moja au nyingine safu hii
imekua msaada mkubwa wa kupindua fikra yako na kukupa uwezowa kuwaza kwa namna
nyingine na kuliendeleza wzo kua endelevu ili uendelee kupata matokeo mapya.
MUHIMU
Haijalishi ni taarifa ngapi potofu ulizozipata mpaka
sasa,na hii inaweza kua kwa kujua au kwa kutokujua.Kitu unachotakiwa kutambua
kua jana imepita na haitarudi tena milele yako yote..yaliyotokea jana huwezi
kuyabadili yatabaki kua historia.Lakini habari njema hapa ni kwamba una maamuzi
makubwa sana juu ya kesho yako,Haijalishi umeharibu kwa kiasi gani katika
maisha yako na haijalishi umesikia nini na umefeli mara ngapi kwa ukosefu wa
taarifa sahihi!JANA IMEPITA LAKINI KESHO IKO MIKONONI MWAKO....Leo ni siku mpya
ya kipekee ambayo ukizingatia maneno haya ambayo pengine unaweza kuyasoma na
kuona ni ya kawaida sana lakinii nakwambia kwamba ni sekunde moja tu ya utii wa
neno inatosha kubadili historia yako.Bado unanafasi ya kuibadili kesho yako kua
ni ya mafanikio ambayo kwa hakika kama utaamua kufanya hivyo itabadili mtazamo
wako na kukufuta machozi yako ya jana pale ulipoanguka na kushindwa.BADILI
CHANZO CHA TAARIFA UPATE MATOKEO MAPYA.
HITIMISHO/SHUKRANI
Leo ndio J3 ya mwisho kabisa katika safu yetu hii ya
hazina ya maarifa msimu wa kwanza ambao tulikua tukijifunza kwa pamoja kitu
kiitwacho....BADILI CHANZO CHA TAARIFA.Haimaanishi kwamba leo ni mwisho wa safu
hii hapana lakini kwa msaada wa Mungu ninaamini katika msimu wa pili wa safu
hii kuna mambo mazuri na makubwa zaidi ambayo yanakuja kwajili yako rafiki
yangu msomaji unaezifuatilia safu zangu kupitia mtandao huu.
Namshukuru sana Mungu ambae yeye ni nafasi ya kwanza
kwangu kwa kunipa kipaji uwezo na kibali cha kuifanya kazi hii,Lakini pia
nawashukuru sana wasomaji wangu wote kwa kua bega kwa began a mimi katika
safari hii.Pia kipekee sana nimshukuru rafiki yangu Jimy temuu ambae ndie
mmiliki wa bolg kwa kulipokea wazo langu na kuniamini kunipa umanja wa kuweza
kuandika katika ukuta huu.Pia marafiki zangu wengine wengi ambao tumekua bega
kwa bega kuufanikisha mzigo huu kwenda hewani...James Kalekwa(PHD) Samuel
sasali Prosper Mwakitalima na kipekee zaidi wewe unasoma hivi sasa.
Unataka kujua msimu wa pili katika safu hii
kunani....? Basi tukutane kupitia ukuta huu huu siku ile ile...........kaa
tayari
KWA MAONI NA USHAURI
Fredymsungu@gmail.com
0653 318117
0798 020103
FACEBOOK ACCOUNT
FRED MSUNGU
WHATSAPP 0653 318117
Mungu akubariki
sana .........
WAPINDUA ULIMWENGU
(MAPINDUZI YA FIKRA)


0 comments: