PASAKA WA PILI NI
UREJESHO WA KUSUDI KUU LA KWANZA LA UFALME WA MUNGU.
Utangulizi
“Sikukuu”
ya Pasaka inatokana (asili yake) na maandiko ya neno la Mungu yaani Biblia
(Rejea kitabu cha Kutoka 12:1-51).
Humo ndimo unapatikana mwanzo wa habari ya Pasaka na namna inavyopaswa kuwa.
Hata hivyo mtazamo wa watu wengi na dunia kwa ujumla juu ya Pasaka umebadilika
sana. Wengi wameichukulia kuwa kama siku, wengine huitambua kama siku na hata
baddhi ya watu huiona kama maadhimisho tu na hivyo kuifananisha na siku,
Sikukuu au maadhimisho mengine ya kawaida kabisa. Jambo la msingi ninalotamani
sana ujifunze katika safu hii ya makutano
ya tai ni kwamba Pasaka ni sadaka wala si siku/Sikukuu/maadhimisho.
Jambo jingine ni kwamba, Pasaka kama sadaka haikutolewa kwa bahati mbaya bali
kulikuwa na kusudi la kutolewa kwa dhabihu hiyo
Ufalme
wa Mungu ni kusudi kuu la uumbaji wa Mungu tangu milele. Mafundisho juu ya
ufalme wa Mungu yamekuwa yakitolewa kwa uchache sana ndani ya kanisa la zama
zetu. Hivyo katika mafundisho haya nitaonyesha jinsi gani Yesu Kristo ambaye
ndiye Pasaka wa pili (1Wakorintho 5:7-8)
alikufa ili kurejesha kusudi kuu la awali la Mungu kwa habari ya
mwendelezo
(extension) wa ufalme wake katikati ya wanadamu (Wakolosai 1:13).
Fuatana
nami katika mafundisho haya na maisha yako hayatakuwa kama yalivyo!
Kutoka
12:1-51
Taifa
teule la Mungu, Israeli walikaa katika hali ya utumwa chini ya ufalme
mwingine (bila kuwa na uongozi wa Mungu) kwa miaka 430 (Rejea Kutoka
12:40b).
Kuwa
mtumwa maana yake kuishi chini au/na kwa utashi wa bwana mwingine (si kama
utakavyo). Na kuwa chini ya ufalme (wa Mungu ama wa ulimwengu) ni kuishi
matakwa/mapenzi ya mfalme aongozaye. Sasa, wana wa Israeli walikuwa chini ya
ufalme, si ufalme wa Mungu, bali ufalme wa Misri uliokuwa ukiongozwa na Farao
(mfalme wa Misri). Maana yake ni kwamba waliishi mapenzi/matakwa ya mfalme
asiye mfalme wao… Kwa lugha nyepesi sana na ya kueleweka, walikuwa ni mateka
(captives).
Waisraeli
walitumikishwa na kufanya kazi ngumu na nzito (Kutoka 1:13-14); watoto wao wa kiume waliuwawa (Kutoka 1:16). Kazi ngumu na nzito
walizofanya zinathibishwa na moja ya maajabu saba ya dunia, yale mapiramidi
(pyramids) ya Misri… Hakuna mashine au mitambo inayoweza kufanya kazi kubwa
kiasi kile – ndiyo maana mapiramidi ni maajabu ya dunia! Waisraeli
hawakuyafurahia maisha wala kuufurahia uumbaji wa Mungu kwasababu walikuwa
katika hali ya utumwa na chini ya ufalme.
Waliozaliwa
na kuikuta hali hiyo, walichukulia kuwa ndiyo kawaida ya maisha kwasababu
hawakuwahi kuijua kawaida nyingine… Utumwa na kuwa chini ya utawala ukawa ni
uzoefu wa maisha yao kila siku (daily experience). Akili yao ikafungwa na mfumo
wa maisha yao ya kila siku hii ikawapelekea kujenga fikra za kitumwa (slavery
mindset/mentality). Walijichukulia kuwa wao ni wa hivi hivi, lasivyo
angepatikana mmoja kati yao ambaye angewaza tofauti na kutafuta suluhu ya
matatizo yao. Akili zao hazikuweza kufikiri maisha nje ya utumwa na ufalme wa Misri (They
couldn’t comprehend what it
feels/means out of bondage and out of Pharaoh’s kingdom)… Hebu nikuonyeshe
jambo muhimu sana hapa, usiruhusu mazingira yako kukuaminisha ya kwamba huwezi
kutoka kwenye hayo! Unaweza kuwa zaidi ya mazingira yanavyosema, unaweza kuwa
zaidi ya hali zinazokuzunguka… Mtanzania umesikia mara nyingi tukiitwa, nchi
maskini, nchi zenye kipato kidog, nchi changa n.k nakuambia katika ujasiri wa
Yesu Kristo unaweza kuwa zaidi ya hapo!
Mateso
ya utumuwa yalikuwa makubwa na makali kiasi kwamba wana wa Israeli hawakujua
wafanye nini zaidi ya kulia kilio kikuu. Hakuna kati yao aliyekuwa na jibu la
matatizo yao (Kutoka 2:23-25). Hawa
ndugu waliona jambo pekee wanaloweza kufanya ili kujinasua kwenye hilo tatizo
ni kulia kilio kikuu!!! Ooh, Mungu akusaidie usiwe kama wao… Hakuna aliyesimama
na kuwahamasisha, hakuna aliyekataa hali hiyo, hakuna aliyewaza mawazo mbadala,
hakuna aliyejitutumua na kujipiga kifua ili kuleta upinzani kwenye hali yao ya
utumwa. Wanaume walilia na wanawake vivyo hivyo; watoto kwa wazee… Kila mmoja
alilia kilio kikuu! Ninachotaka uone hapa ni kwamba, kulia hakusaidii jambo
lolote, kujihurumia au kulalamika hakuondoi hata chembe/nukta ya “utumwa”…
Mpaka mtu asimame afanye jambo!
Na
baada ya hapo tunaona Mungu anaingilia kati na kuanza mpango wa kuwakomboa wana
wa Israeli kutoka katika hali hiyo mbovu. Jambo ambalo moyoni mwangu ninatamani
ulione kwa
Mtayarishaji na mwandishi wa makala haya ni mwanataaluma na
mwalimu.
Kwa mawasiliano zaidi:
James Kalekwa
+255 754 917 764
+255 714 762 669
kalekwajames@gmail.com
Kwa mawasiliano zaidi:
James Kalekwa
+255 754 917 764
+255 714 762 669
kalekwajames@gmail.com
Amen! Ni Bwana!
ReplyDelete