Monday, April 28, 2014

KUTOKA MOSHI HILI NDILO KANISA LILILOJENGWA NA MKOLONI LIKIWA NA MIAKA 82.

By Jimmy  |  11:50 AM No comments


Kutoka Moshi usharika wa Lyamungo  kati jimbo la kaskazini,dayosisi ya kaskazini hili ndilo kanisa lililojengwa na mkoloni linalo semekana kuwa na miaka mingi likiwa bado liko
imara japo kwa sasa alitumiki tena.....kutoka kwa ripota wangu Everlight aliyeko Moshi ameifahamisha blog kanisa hili lilijengwa tarehe 17/10/1932 na kupewa jina la TEREVEN maana yake ombeni au kwa lugha ya kiebrania ROGATE,ni kanisa lililo jengwana na wakoloni ila kwa sasa Kanisa hili alitumiki baada ya Askofu Martin Shayo kuwaambia waamie jengo la kanisa jipya likiwa bado  halijakamilika.

 Kanisa jipya likiwa bado kwenye matengenezo.
 Siku ya jana katika ibada ya J/pili kulifanyika harambee ya kukusanya pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa ambapo mgeni rasmi alikuwa YESU mwenyewe ambapo  muendesha shughulia MC Heavenlight Massawe alichukua kiti na kukiweka mbele ya madhabahu na kutamka leo katika harambee hii hatuna mgeni rasmi hivyo mgeni rasmi yuko hapa mbele ni YESU mwenyewe hivyo na mkaribisha akae na kisha akaendelea na kazi yake.
Kwaya ikiimba.
 Kanisa jipya lilianza  kujengwa mwaka 2009 linatarajiwa kumalizika mwaka 2017 Mungu akipenda...kanisa hilo jipya linakadiriwa kuchukua watu 2500 kwa wakati mmoja.
 Kushoto ni Mwenyekiti wa jengo mzee Matinga akiteta jambo na mzee wa kanisa.

 Mc akiendelea na harambee

Ukimuangalia MC mbele yake kuna kiti.....hicho kiti ndicho alichopewa mgeni rasmi "YESU" mpaka ripota wangu Everlight anatoka mahali hapo kulipatikana pesa milioni 12.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP