SAFU
YA FRED MSUNGU: BADILI CHANZO CHA TAARIFA
JINSI
ULIVYO LEO NI MATOKEO YA ULICHOKISIKIA NA KUKIAMINI
FIKRA TATA: 1
i.
Hakuna mtu aliezaliwa
na kitu/mali /mafanikio... Inaweza ikakupa shida kuamini kwasababu kila siku
unaona kuna watu mashuhuri/matajiri na wana watoto, utaniambia Fred wale si
watu waliozaliwa na kuyakuta mafanikio tayari? Ni sawa lakini hebu tulia kidogo
na fikiri hivi yule mtu wa kwanza kabisa ambae ndio mwenye hayo mafanikio ...Je
nayeye hizo mali/mafanikio alizitoa wapi? Jibu ni rahisi sana hapa kwamba
wakati wote tulikua katika hali sawa uwezo sawa na mazingira sawa kuna mtu
mmoja ambae yeye aliamua kufikiri zaidi ya mipaka ya kawaida (fikra nje ya
boksi) Matokeo ya kufikiri nje ya mipaka ni kufanya vitu nje ya mipaka na
kufanya vitu nje ya mipaka ni kupata matokeo makubwa nje ya mipaka.Baada ya
hayo yote sasa utofauti ndio unaanza kuonekana kwasababu yeye aliamua kulipa
gharama na kutenda nje ya mipaka ni lazima matokeo yamtoe nje ya mipaka pia na
ndio maana watu wenye uwezu wa juu na wasio na uwezo hawakai sehemu moja..Unaweza
ukalahumu saaana lakini mfumo ndo umeamua hivyo aliwaza nje ya mipaka ataishi
nje ya mipaka pia, Lakini wote mwanzo wetu ulikua sawa.
AMKA
MAISHA NI UCHAGUZI.
KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MALENGO/NDOTO NA TAARIFA?
Hili linaweza kua
moja kati ya maswali ambayo umejiuliza sana toka ulipoanza kusoma safu hii,
Kwamba mipango /ndoto ni yako wewe binafsi sasa taarifa inaingiaje hapa ama
kuna uhusiano gani baina ya vitu hivi viwili?
Jibu: Ni kweli
kwamba maisha ni yako wewe ndoto/mipango na maono uliyonayo ni vyako.Lakini
kumbuka mpaka vitu hivyo vikatokee kuna mchakato fulani ambao ni lazima uupitie
kama njia ya kuielekea hatma yako au kilele cha mafanikio yako.
Njia hizo ni:-
I.
Kujifunza/kupata uzoefu:
Sehemu yeyote duniani kwenye sekta yeyote hakuna mtu ambaye amefanikiwa na
akasema kwamba hakuna mtu yeyote mwenye mchango katika mafanikio yake, abadani
si kweli.... mara zote hua kuna watu waliotutangulia (wenye uzoefu)ambao
wamefanya vitu sawa na tunavyoviwaza wakafanikawa, watu hao husimama kama
mifano/ushuhuda kwa vizazi vingine vijavyo
ili kuyafikia malengo.Kama kumbu kumbu yako nzuri utakumbuka mwanzoni
kabisa nilikuambia kwamba jitambue wewe ni nani na unataka nini ili uchague
watu unaodhani wanafanana na wewe ili upate uzoefu(kujifunza toka kwao)Ili
kuyafikia matokeo unayoyatarajia.Na uzoefu huo utaupata kwa njia ya kujifunza.
Kuna njia nyinginezo
nyingi ambazo ni vyanzo vya taarifa, Na huu ndio uhusiano sasa kati ya ndoto
yako/malengo/mipango na taarifa. Taarifa inaathiri Sana matokeo ya malengo yako
kwasababu wakati wa kutendea kazi mawazo unazungukwa ka watu mbali mbali na pengine
ili kufikia malengo itakuhitaji pia kuwatumia baadhi ya watu ili kutoboza
upande wa pili na hii ndio sababu unatakiwa kua na chanzo sahihi cha taarifa
ili usikie vitu sahihi.
UMECHAGUA FUNGU GANI LA TAARIFA!
Kama swala la
kusikia! Watu wengi wanasikia.....Ila unasikia nini? Kutoka Kwa nani? Hapa ndio
nataka kujenga hoja yangu Kwa upana kwasababu chochote ulichoamini mwanzo wake
ulikua ni kusikia. Baada ya kusikia na kuamini maamuzi ya vitendo hufuata.Na
hapa ndipo safari ya mafanikio au ya kufeli (kutofanikiwa)inaanza.Na hii
inatokana umesikia taarifa gani kutoka
kwenye chanzo gani uliochagua
kuisikiliza na kuiamini.Ukisikia taarifa sahihi utaamua kwa jinnsi ilivyo
sahihi ,Pia ukisikia kwa taarifa isiyo sahihi kutoka kwenye chanzo kisicho
sahihi basi fikra na maamuzi yako pia
hayatakua sahihi.Inawezekana kabisa ukaona ukuu ndani yako ukawa na mipango
mikubwa tu , lakini kama utaruhusu masikio na fikra yako kupokea taarifa za
kushindwa mara kwa mara, haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani ukiruhusu
taarifa za kushindwa tegemea kushindwa pia.
Kabla sijatoa
mfano huu nikuweke sawa kwanza katika hili...Kwagu mimi kiwango cha utajiri wa
mtu au mafanikio makubwa ya aina yeyote si kigezo kwamba Mungu ndio anatenda
kazi au niamini Mungu kwasababu amefany litu fulani,Nimefika mahali pa kuelewa
kua Mungu hua anabaki kua Mungu tu iwe ametenda unachotaka au hajatenda..(Mungu
hapimwi kwa alichofanya anabaki kua Mungu kwasababu ndivyo alivyo) huo ni
mtazamo wangu, Japo kua mimi siamini katika umasikini
Sasa mfano wangu
ni huu..!Ukifanya tathinimi ya wale wachungaji ambao wao wanahubiri sana injili
za aina moja unyonge (uhitaji) hebu jaribu kuangalia maisha yao na ya watu
wanaowaongoza...hali zao kiuchumi (kimaisha)hua ni mbaya sana na wao hua
wameridhika kabisa , Lakini si kwamba Mungu hawezi kufanya kitu au hawana Mungu
hapana! Ila kwasababu ni kitu ambacho wanakisikia kwa sana,Hivyo inawajengea
imani na imani inaleta matokeo ya walichokisia.Kwahiyo hili si swala la kumlaumu
mtu ni swala la ufahamu tu...Baba wa upentecoste Nigeria Askofu mkuu Benson
Idahosa enzi za uhai wake aliwahi kusema
hivi ‘Ukihubiri sana juu ya habari ya kuzimu(moto) kuna hatari kubwa washirika
wako wakaishia huko,Lakini ukihubiri sana juu ya habari za mbinguni kuna
asilimia kubwa ya watu unaowaongoza kuiona mbingu(peponi)’.Kauli hii ilinigusa
sana na imeakisi sana ujumbe wangu kwamba chanzo cha taarifa kikiwa kibaya mara
kwa mara tegemea matokeo mabaya na pia ukijizoesha kusikiliza taarifa za
ushindi tegemea ushindi pia.
Hata katika
maisha yetu ya kawaida kabisa kuna watu wengi waliamua kufanya vitu kutokana na
taarifa fulani waliosikia kwa wengine. Aina hii ya taarifa tunaweza kuiita ni
ushuhuda. Mfano: Watu wengi katika biashara ya simu mara nyingi wanahama katika
mitando yao kwenda mitandao mingine kwasababu ya kusikia taarifa(ushuhuda)toka
kwa mwingine kwamba huku kuna nafuu kuliko sehemu nyingine.Kinachomfanya huyu
mtu kufanya maamuzi ya kuhama ni ile taarifa (ushuhuda)aliyoipata kutoka kwa
mwingine,Hivyo maamuzi yake yameathiriwa na taarifa aliyoisikia.
Mfano: 2 Watu
wengi sasa wanaamua kuondoka vijijini kukimbilia mjini kutokana na taarifa
wanazozipata kwamba mjini kuna maisha mazuri kuliko kijijni.Inawezekana ikawa
si taarifa sahihi lakini tayari mtu kashafanya maamuzi kutokana na aina ya
taarifa aliyoipata.Hata makanisani watu wanahama kutokana na taarifa
wanazozipata zinazowapelekea wao kuamini kwamba kuna matokeo tofauti
atakayoyapata, Haijalishi kama lengo hua linatimia au halitimii....kikubwa hapa
ni kwamba kitu kilichomsababisha mtu kufanya maamuzi aliyofanya ni ile taarifa
aliyoipata.Somo hili litaendea J/tatu ijayo,usikose kuendelea kufatilia safu hii iliyoandaliwa na Fred Msungu.Kwa mawasiliano zaidi piga simu No 0653-318117 au fredymsungu@gmail.com.
0 comments: