Nani mwenye haki ya kuuza nyimbo za
Marehemu Anjela Chibalonza?Je Ni Mama yake mzazi? Dada yake? Au aliyekuwa mume
wake Pastor Elisha Muliri ambaye kwa sasa ameshaoa.....
au Mke mwingine?Ugomvi mkubwa umezuka kati ya Mmoja wa Dada wa Marehemu
Angela Chibalonza na Bwana Muliri aliyekuwa
mume wa Angela,ambapo kila mmoja anachodai ni haki yake kuuza nyimbo za
marehemu.
Hali ni tete kiasi cha Muliri kutisha kuua Shemeji
yake kama hata koma kuuza nyimbo za Marehemu ambaye Muliri anadai ni mke wake na
Shemeji anadai ni dada yake.Kwa maoni yako nani kati yao mwenye haki zaidi ya
mwingine kuuza nyimbo za Marehemu Anjela Chibalonza?Dada anamwambia Muliri kifo kiliwatenganisha na
umeoa mke mwingine kwa hiyo Angela siyo mke wako kwa sasa na nyimbo zake
sisi familia ya Angela ndio tuna haki kuziuza.Naye Bwana Muliri anasema mimi na Anjela tulioana
tukawa mwili mmoja hivyo nina haki..
Chanzo cha taarifa Munishi Faustin.
0 comments: