SAFU
YA FRED MSUNGU: BADILI CHANZO CHA TAARIFA
JINSI
ULIVYO LEO NI MATOKEO YA ULICHOKISIKIA NA KUKIAMINI
SEHEMU YA TATU.....
FIKRA TATA: 2
Siku za hivi
karibuni kuna uvumi umechukua umaarufu sana kwenye akili za watu na kwenye
vichwa mbalimbali vya habari juu ya watu
wenye mafanikio makubwa.Imani za watu wengi sasa zimejengeka kwamba haiwezekani
mtu kufanya kazi au kua na bidii katika eneno lake na akafanikiwa bila
viambatanishi vya ziada,Hivyo uchawi umevuma sana kua ni chanzo cha mafanikio kwa watu wengi.Wengine
wamekwenda mbali zaidi na kuanza kuongea habari za freemason na kuwahusisha
watu kadhaa waliofanikiwa na tuhumma
hizo,Hii imechangia sana kupunguza mori na ufanisi wa watu katika utendaji
wakiamini kwamba ukitaka mafanikio haiwezekani bila kujiambatanisha na hivyo
vitu.Binafsi niko kinyume sana na dhana hiyo,sipingi kwamba uchawi upo na
kwamba kuna watu wanaofanikiwa kwa njia zisizo halali...la hasha! lakini
ninachopinga hapa ni watu kujipa dharula na kupunguza ufanisi na kukaa chini
kuwaza kwamba watu wengi wenye mafanikio wanajihusihsa na mambo haramu
kama
hayo.Kwa mtazamo wangu kama wewe ni mtu wa maono na ndoto kubwa katika maisha yako kuhusisha mafanikio ya mtu na
uchawi,freemason au nguvu nyingine ya ziada sidhani kama hicho ni chanzo kizuri
cha taarifa kwako.Mtu yeyote mwenye ndoto au matarajio makubwa mara zote huwaza
chanya na sio hasi.Maana kama haiwezekani kufanikiwa bila kujihusisha na vitu
hivyo basi inamaanisha na wewe hautaweza kufikia malengo yako .Mtu mkuu huwaza
mambo makuu ndani yake na mambo makuu ni yale tu yanayotokana na fikra sahihi
(chanya) Hivyo ushauri wangu kwako ukiwa
na ndoto za ukuu ndani yako achana na mawazo ya watu wanaovumisha mambo yasio
na manufaa,Ongeza juhudi, maarifa,kaa kwenye lengo na pokea taarifa sahihi
kutoka kwenye chanzo sahihi utapata matokeo sahihi.
(Hagai 2:8) Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali
yangu asema bwana wa majeshi. Andiko
hili linabeba maana nzima ya mafanikio japo hapo ameongelea kuhusu fedha na
dhahabu,Sasa kama fedha nadhahabu ni mali ya baba yako maana halisi hapa ni
kwambaunanafasi ya urithi katika vitu hivyo.Ni swala la kujitambua tu na
kuchukua hatua ya kufanya wajibu wako ili upate haki yako. HAKUNA HAKI BILA
WAJIBU...Hii ina maana kuna mambo ambayo ni lazima uyafanye kwanza ili kwayo
upate kumiliki.
I.
NINI
CHANZO SAHIHI NA NINI SI CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA
Jibu la swali
hili linategemea sana na maisha uliyochagua (hatma yako) na aina ya malengo
uliyonayo.Inawezekana sana chanzo hicho hicho kikawa ni sahihi sana kwa wengine
lakini kwako kisiwe ni sahihi,Naweza nikawa nimekupa wakati
mgumu wa kufikiri lakini kadri unavyozidi kusoma ndivyo fikra yako inapanuka na
ninaamini mpaka mwisho tutakua kwa pamoja tumeipata maana halisi ya somo hili.
MUHIMU: Jambo la
muhimu sana kujua hapa ni hili ‘ Huwezi kuja kuyafikia matokeo makubwa zaidi ya
fikra zako zinavyoona....Jinsi vile unawaza ,unaona juu yako na juu ya kesho (hatma)yako
ndivyo vile utakavyokua.Hakuna muujiza wala uchawi wa aina yeyote katika hili
,Kipimo au kiwango ulichonacho juu yako ndicho hicho utakua milele.(Mithali 23:7 )Ajionavyo mtu nafsini mwake
ndivyo alivyo.
Ukiisoma hiyo
mithali utaona hapo ametumia neno ‘Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo’
Naliangalia kwa jicho la tofauti sana neno NDIVYO ALIVYO!Maana ninayoipata hapa
ni kwamba kile unachokiona ndani yako haijalishi kimekwisha kutokea
(kudhihirika)au bado hakijatokea lakini vile unaona ndivyo ulivyo.Maana yake
hapa kama unaona ukuu ndani yako tayari wewe ni mkuu ila kuna hatua ambayo
unatakiwa kuifanya tu ili kudhihirisha ile hali ilio ndani yako iwe katika
ulimwengu halisia.Moja kati ya hivyo kupata chanzo sahihi kitakacho kuwezesha
kuthibitisha hali yako ya ndani nje.Pia kama unaona madhaifu ndani yako maana
yake hivyo ndivyo ulivyo kwasababu hicho ndicho unachoona.Mtu alie na ukuu
ndani yake ana kazi ya kuuthibitisha maana matokeo ya ukuu hayawezi kuonekana
wala kufaidia kitu mpaka yamethibitika kwa watu wengine.Lakini mtu unaeona
mapungufu(mpumbavu) ndani yake wala hana kazi yeyote ya kukuthibitishia maana
utamuona tu jinsi anavyoishi,anavyo waza na hata usemi wake tu utamuelewa huyo
ni mtu wa namna gani.
FIKRA TATA: 2
Siku za hivi
karibuni kuna uvumi umechukua umaarufu sana kwenye akili za watu na kwenye
vichwa mbalimbali vya habari juu ya watu
wenye mafanikio makubwa.Imani za watu wengi sasa zimejengeka kwamba haiwezekani
mtu kufanya kazi au kua na bidii katika eneno lake na akafanikiwa bila
viambatanishi vya ziada,Hivyo uchawi umevuma sana kua ni chanzo cha mafanikio kwa watu wengi.Wengine
wamekwenda mbali zaidi na kuanza kuongea habari za freemason na kuwahusisha
watu kadhaa waliofanikiwa na tuhumma
hizo,Hii imechangia sana kupunguza mori na ufanisi wa watu katika utendaji
wakiamini kwamba ukitaka mafanikio haiwezekani bila kujiambatanisha na hivyo
vitu.Binafsi niko kinyume sana na dhana hiyo,sipingi kwamba uchawi upo na
kwamba kuna watu wanaofanikiwa kwa njia zisizo halali...la hasha! lakini
ninachopinga hapa ni watu kujipa dharula na kupunguza ufanisi na kukaa chini
kuwaza kwamba watu wengi wenye mafanikio wanajihusihsa na mambo haramu kama
hayo.Kwa mtazamo wangu kama wewe ni mtu wa maono na ndoto kubwa katika maisha yako kuhusisha mafanikio ya mtu na
uchawi,freemason au nguvu nyingine ya ziada sidhani kama hicho ni chanzo kizuri
cha taarifa kwako.Mtu yeyote mwenye ndoto au matarajio makubwa mara zote huwaza
chanya na sio hasi.Maana kama haiwezekani kufanikiwa bila kujihusisha na vitu
hivyo basi inamaanisha na wewe hautaweza kufikia malengo yako .Mtu mkuu huwaza
mambo makuu ndani yake na mambo makuu ni yale tu yanayotokana na fikra sahihi
(chanya) Hivyo ushauri wangu kwako ukiwa
na ndoto za ukuu ndani yako achana na mawazo ya watu wanaovumisha mambo yasio
na manufaa,Ongeza juhudi, maarifa,kaa kwenye lengo na pokea taarifa sahihi
kutoka kwenye chanzo sahihi utapata matokeo sahihi.
(Hagai 2:8) Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali
yangu asema bwana wa majeshi. Andiko
hili linabeba maana nzima ya mafanikio japo hapo ameongelea kuhusu fedha na
dhahabu,Sasa kama fedha nadhahabu ni mali ya baba yako maana halisi hapa ni
kwambaunanafasi ya urithi katika vitu hivyo.Ni swala la kujitambua tu na
kuchukua hatua ya kufanya wajibu wako ili upate haki yako. HAKUNA HAKI BILA
WAJIBU...Hii ina maana kuna mambo ambayo ni lazima uyafanye kwanza ili kwayo
upate kumiliki.Somo
hili litaendea J/tatu ijayo,usikose kuendelea kufatilia safu hii
iliyoandaliwa na Fred Msungu.Kwa mawasiliano zaidi piga simu No
0653-318117 au fredymsungu@gmail.com.
0 comments: