KOMPYUTA zinazotumia windows XP
hazitoweza kupokea taarifa muhimu na kuongezeka mashambulizi ya virusi vya
spyware vinavyoharibu taarifa binafsi na takwimu za kibiashara baada ya mwezi
mmoja. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Microsoft kwa kanda
za Afrika Mashariki, Magharibi, Rotimi Olimide
Alisema kuwa utafiti mpya
wa Microsoft umeonyesha kuwa Window XP hushambuliwa kirahisi na virusi mara tano zaidi huku usalama wake ukiwa mdogo kiasi cha kuruhusu wizi wa mtandao.
wa Microsoft umeonyesha kuwa Window XP hushambuliwa kirahisi na virusi mara tano zaidi huku usalama wake ukiwa mdogo kiasi cha kuruhusu wizi wa mtandao.
Alisema ni vyema ndani ya mwezi
mmoja, watumiaji wa window hiyo wakabadilika na kuhamia Window 8 ambayo ina
uwezo mkubwa wa kuhimili mshambulizi ya virusi.
“Mfumo uliotengenezwa kwenye Window
XP ni wa kizamani na uendeshaji wake sio iliyoundwa kujilinda dhidi ya virusi.
“Baada ya mwezi mmoja si kuwa huduma
ya Window XP haitafanya kazi, unaweza kuendelea nayo lakini usalama na utendaji
wake hautakuwa mzuri ,” alisema.
Alisema mfumo wa uendeshaji wa
Windows 8 na Office 365 unatoa ulinzi wa uhakika na ufanisi. Mkurungezi wa Teknolojia
na Uendeshaji, Chege Thumbi alisema ni vyema hasa taasisi za kifedha kuacha
kutumia windows XP mara moja ili kuwa katika usalama na urahisi wa kufanya
biashara.
0 comments: