Tuesday, February 18, 2014

KUSIFU NA KUABUDU

By Unknown  |  10:45 PM No comments

NAMNA YA KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU

                                                                                                               

Na ili kumpa Mungu sifa na ibada, ni lazima na ni muhimu sana ujue
mambo ambayo yanamstahilisha Mungu wetu kusifiwa na kutukuzwa. Kwa
kutumia sifa na tabia za Mungu, utaweza kumsifu na kumwabudu vizuri.
Hakuna kiumbe kingine chochote kinazo zile sifa kuu tano za Mungu,
isipokuwa yeye Mungu Jehova peke yake.Unapomueleza Mungu sifa zake na tabia zake (vile alivyo) hapo unakuwa unamsifu na kumwabudu.

 Lakini tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako
au sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, kusifu na kuabudu
na kushukuru, ni mambo yanayofanyika kwa kuingliana sana.

kusifu, kushukuru na kuabudu, ni mambo
yanayofanana sana. Inaweza ikawa vigumu kidogo kuyatenganisha kimaelezo
au kivitendo. Ni ngumu kidogo, kufanya kimoja pasipo wenzake, kwasababu ni
mambo yanayokwenda kwa pamoja sana. Lakini kwa tafsiri zake, yako hivi;

1. Kumshukuru Mungu;‐ Ni ile hali ya kumueleza Mungu jinsi
tunavyothamini (Appreciate and Admire) wema wake, fadhili zake na
baraka zake katika maisha yetu.
2. Kumsifu Mungu; ‐ Ni kumueleza Mungu juu ya matendo yake makuu
na ya ajabu aliyoyafanya. Au ni kuwaeleza wengine kuhusu matendo
makuu ya Mungu aliyoyafanya katika maisha yetu au kwa watu
wengine.


Photo: CHURCH MINISTRY 

3. Kumwabudu Mungu; ‐ Ni kumueleza Mungu tukuzo zetu, heshima yetu
na upendo wetu kwake kwasababu ya uzuri wa tabia zake kwetu.
(Credentials and Characters).

Kwahiyo, tuendapo mbele za Mungu kwa ibada, iwe ni chumbani kwako au
sebuleni kwako au kwenye gari lako au kanisani kwako, ili kumsifu na
kumwabudu na kumshukuru Mungu, uwe huru kujimimina mbele za Mungu
kwa kufanya vyote vitatu, kwa namna moyo wako utakavyokuwa unaongozwa
na Roho Mtakatifu. Vyote vitatu vinatengeneza ibada takatifu kwa Mungu.


Kwahiyo, utengapo muda wa kukaa mbele za Mungu wetu
kwa ibada, msifu na kumtukuza Mungu kwa mambo yafuatayo,
1. Mtukuze Mungu kwa Sifa zake za Uungu (ambazo hakuna mwingine
aliye nazo) Kwamba;
a) Jehova ni Mungu wa Milele
b) Jehova ni Mungu Mtakatifu
c) Jehova ni Mungu Aliye kila mahali
d) Jehova ni Mungu Anayejua mambo yote
e) Jehova ni Mungu Aliye na nguvu zote na
anaweza kufanya mambo yote kabisa.

Photo: At Nsumba Prayer Ground
Blogger of Apostle Darmacy

 


Author: Unknown

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP