Thursday, October 17, 2013

KUTOKA FACEBOOK HUU NDIO MTAZAMO WA WADAU KUHUSU MFARAKANO WA TAG na EAGT.

By Jimmy  |  9:58 AM No comments

Mussa Billegeya 
 
Nilikuwa naangalia ITV, Taarifa za Idd-E-Haj huko Kigoma, MASHEIKH wakasema walikuwa na mafarakano (Mfaraka), lakini wakakaa Pamoja, wakaisuluhisha hiyo mifarakano kwa kutumia SHERIA ZA MWENYEZI MUNGU ambazo Ziko kwenye Quran, na Sasa Wanashirikiana kwa Amani na Mshikamano! Nilisikia TAG na EAGT walikuwa/watakuwa na kesi MAHAKAMANI kuhusu "MGOGORO" baina yao. Wachungaji wangu na Ma-askofu wangu Sylvester Gamanywa, Peter Mitimingi, Matthew Sasali, Florian Katunzi (na wengine) NINAFAHAMU Mungu amewajalia HEKIMA NA BUSARA ZA KIMWILI NA KIROHO, naomba muwashauri MAASKOFU wa TAG na EAGT Waende WAKAJIFUNZE KWA MA-SHEIKH WA KIGOMA namna ya Kumaliza Migogoro ya Kidini kwa Kutumia Vitabu vya Dini, na kama WAKIONA BIBLIA HAIWATOSHI KUJIBU TOFAUTI ZAO MPAKA WAENDE MAHAKAMA ZA KIDUNIA, Basi Washauriwe hata namna ya KUTUMIA QURAN Kumaliza Mgogoro wa TAG na EAGT bila Kwenda Mahakamani - Itakuwa ni Hekima zaidi kuliko AIBU wanayolitia Kanisa kwa Sasa!!!!!! SHAME
  • Richard Zuberi Nanukuu " na kama WAKIONA BIBLIA HAIWATOSHI KUJIBU TOFAUTI ZAO MPAKA WAENDE MAHAKAMA ZA KIDUNIA, Basi Washauriwe hata namna ya KUTUMIA QURAN Kumaliza Mgogoro wa TAG na EAGT bila Kwenda Mahakamani", Bonge la wisdom hilo Mussa.

  • Baba Xtina Biblia utaielewa kwa kusoma mwenyewe c kwa kusomewa!

  • Frank Makelemo kesi ilishaondolewa mahakamani wiki 1 imepita sasa na hayo mambo yanasuluhishwa kikanisa, jaribu kuwa unapata updates kwanza kabla ya kupost vi2 ukiwa kifua mbele. au ulikuwa na lengo lingine mahsusi kwa hiyo post.

  • Andrea Muhozya Washauriwe kutumia QORAN?? People, since when did TWO WRONGS MAKE IT RIGHT? Yaani wamefanya kosa la kwenda Mahakama za kidunia halafu tuwashauri kwenda kwa Qoran? Na hili litakubaliwa na Mungu gani wapendwa? No, no, no. Kama wakishindwa kushaurika kuhusu kutoendelea na mahakamani waliko sasa hivi kilichobaki ni kuwaombea tu. Na kama kanisa kweli tukiomba kwa pamoja in one accord kwa hili Mungu wetu atatujibu!

  • Fredrick Mulinda Kwa hiyo post ya Musa Billegeya ninachoweza kusema ni AMINA. Andrea Muhozya, kama wamekwenda mahakama za kidunia, si afadhali zaidi kupata ushauri wa mashekhe ambao angalau wanamtafuta Mungu japo kwa kupapasapapasa? Unafikiri wanatofautiana sana? Frank Makelemo, asante kwa taarifa hiyo.

  • Andrea Muhozya Fredrick Mulinda hivi ni kweli kabisa kwamba hii ndo busara ya mwisho kabisa kwa wwatu wa Mungu? I am surprised! Ipo siku watumishi wa Mungu watakosea wataambiwa waende kujifunza kwa mganga wa kienyeji namna ya kumaliza tofauti zao. Hivi neno la Mungu halina majibu kwa hali ilipofikia, hakuna hekima kwa kanisa la Mungu mpaka mtoe aina hizo za ushauri? hebu MSHINDWE!

  • Honery Yothamu Mnyanyi Waende, rukhusa kwenda kujifunza hekima ya huko, biblia hajakakataza kujifunza hekima kwao, maana huko kuna mambo mengine hufanyika kwa hekima kuliko hata kwa wana wa nurun, barikiwa dr kuwa-reference huko

  • Fredrick Mulinda Ndg. yangu Andrea Muhozya, kweli TUSHINDWE (hasahasa mimi). Wewe USHINDE! Binafsi sihitaji kushinda ktk hilo unalolitetea. Wewe unafikiri ushauri haukutolewa kabla? Je, neno la Mungu yupi unataka litoe majibu kama si yule anayedhaniwa kwamba wanamtumikia? Mbona hawakumsikiliza kabla ya kufanya uamuzi wa kipumbavu kama huo? Ubora wa "mungu" wa watu wa jinsi hiyo zaidi ya yule wa masheik na waganga wa kienyeji uko wapi? Je, mahakama ilipotupilia mbali madai hayo kwa muda ili mazishi yafanyike kwanza haiku-prove wiser kuwapita? Je, ni kwa sababu mahakama ilitafuta neno la Mungu wa kweli? Aaah, Sometimes we think we are spiritual when we are only religious!

  • Alexander Wenceslaus Andrea ungekua unamfahamu vilivyo Mussa na alichokiongea hapo nadhani usingekurupuka kwenye comment yako ya kwanza. Hiyo ni aina ya uandishi ili kuweka msisitizo. Ni kama Sarcasm. Haimaanishi amekusudia direct kuwa hicho kitabu kingine kitumike kusuluhisha gogoro hili. Ameweka msisitizo yaani kama hekima za ndani zimeshindikana basi waazime zile za wenzao walioweza kusuluhisha farakano lao. Tafakari kwa sauti kabla hujaweka maandishi yako vidoleni.

  • Atupakisye Mlawa mungu wetu hashindwi jambo jamani,naomba tusijisahau kiasi hicho,kwanza toba kisha maombi.kama umebarikiwa sema ameeen!

  • Fanuel Mulinda Teh teh teh. Watumishi wa Mungu hao! mahakamani. Mnatia aibu na kujiachia uchi kwa dunia.

  • Joel Msella Napita tu wajameni!

  • Mussa Billegeya Andrea Muhozya hukuelewa...., Frank Makelemo, asante kwa updates, kumbe nilipaswa kupost huu ushauri kabla hawajaitoa hiy kesi mahakamani, maana Kitendo cha Kuipeleka Mahakamani NDIO ULIKUWA UKOSEFU WA BUSARA, Kuitoa ni busara pia - japo ni busara iliyochelewa! Asante kwa Alexander Wenceslaus kwa ufafanuzi, Fredrick Mulinda tuko pamoja.... HILI HALIKUPASWA KUTOKEA, NA LINATAKIWA LIISHE MARA MOJA!

  • Mussa Billegeya Joel Msella safari njema kaka, Mungu akutangulie!! teh

    Fredrick Mulinda Joel Msella, kama unapita kidigitali lazima uache alama. Sasa we utafikiri umepita kwa ndege bwana, duh hahahaha!


Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP