Monday, October 22, 2012

SAFARI YAKUTOA MILIONI 12 KWA MSHINDI WA TANZANIA WORSHIP EXPERIENCE ZIMEBAKI SIKU 33 KUELEKEA KWENYE FAINALI DIAMOND JUBILEE.

By Jimmy  |  12:27 PM No comments

Hili ni shindano kubwa la kutafuta waabuduo halisi kupitia show kali ya Tanzania worship Experience inayo rushwa kila J/mosi TBC-1.Siku ya J/mosi ya Tarehe 21/10/2012 nimepata kibali kuwa presenter wa show hii kubwa na kali inayo tizamwa  kupitia TBC-1 saa Tatu kamili usiku.Kwa sasa Tanzania worship Experience imefikia katika Top ten kwa washiriki wanao shindania Milioni 12 za kitanzania.

Kazi ya kurecord kipindi hiki huchukua zaidi ya masaa 6 ambapo washiriki wote uimba live kupitia band kali yenye viwango vizuri na vya hali ya juu.Nikiwa na Presenter mwenzangu Debora siku ya J/mosi tulinya kweli kupitia washiriki walio ingia Top ten.

Huu ni mchuano mkali kuelekea fainali Tarehe 25/11/2012 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.Tanzania Worship Experience kupitia kipindi chake kinacho rushwa kila J/mosi TBC-1 wametoa nafasi yakumpigia kura kila mshiriki aliye ingia 10 bora.
 Kadiri utakavyo piga kura nyingi utajishindia Simu ya mkononi kupitia Tanzania Worship Experience kila J/mosi kupitia runinga yako ya TBC-1.Jinsi ya kushiriki kupiga kura yako kwa mshiriki wa kwanza hadi wa kumi,nenda sehemu ya simu yako ya kutuma ujumbe andika T W E acha nafasi andika namba ya mshiriki kisha tuma kwenda namba 15678.

Kumbuka fainali za shindano hili linalo rushwa na kituo cha TBC-1 zitafanyika Tarehe 25/11/2012 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.Lakini kumbuka kipindi hiki hukujia kila J/mosi saa Tatu kamili usiku 
 On set kabla ya record
 Big bosiiii Bilionea
 On set
 Kushoto Mr Makaranga coordinator wa Show,Debora & Uncle Jimmy presenter wa Tanzania Worship Experience
 Hapa sijui nilikuwa naeleza nini vilee!!
 Partner wangu Debora akiuza maneno siku ya J/mosi 



Poziiiiiiiii  Jessica
HIKI NI KITUKO NILICHO KIPENDA KWA MTOTO WA MCH DEO LUBALA.
Abby Lubala akiiyanza safari ya kupeleka vyombo njee baada ya show kumalizika.
 Kupiga jicho mbele akamuona Swahiba yake Baraka Paul na kitololi cha kubebea mizigo,asiombe lifti.
 Tazama alivyo pewa kampani yakutosha na Baraka Paul.
 Kama movie vileeee
 Baada ya kumshusha Baraka akaendelea na kazi.
Hawa ndio walio ingia kwenye Top ten ya Tanzania Worship Experience


Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP