Kuna watu maarufu hapa mjini lakini
kuna maarufu wa Facebook.Unaweza usinielewe katika hili lakini wao
chochote wanacho andika katika Walls zao wana watu wengi ambao hupita
nakutoa Comments zao.Wapo ambao wakiandika hata ujinga au kichekesho
lazima watu watatoa Comments zao.
Leo
naomba nikulete baadhi ya watu maarufu katika Facebook ambao hapa
mjini wana mashabiki kedekede pale wanapo andika jambo lolote katika
Walls zao.Kama kuna wengine unawajua tafadhari nifahamishe katika kiboksi
cha "Lets Chart Here" pembeni mkono mwakushoto wa Blog
WATU 6 MAARUFU KATIKA FACEBOOK
Masanja Mkandamizaji.
Huyu
kwangu atakuwa mtu wa kwanza {No1}ambaye yeye huandika vichekesho na
vituko. Mara anapo andika upita watu wengi kutoa Comments zao.Kama kuna siku
umeamka hauko vizuri na una hitaji kucheka na kupunguza msongo wa mawazo
pita kwenye wall yake ufurahi na roho yako.
Mfano wa watu wanao comment kwenye wall yake.
Blogger Sam Sasali
Kijana
huyu mtoto wa Pastor yeye huwa hatabiriki hata siku moja.Yeye ukimleta kwenye
ishu za Siasa yupo,Vituko yupo vitu siriazi vya maisha ndio usiseme.Na
kwa sasa anamtindo wake wa kuanza na maneno ya Tenzi za Rohoni pale
kunapokucha asubuhi.Ukiingia tu kwenye Wall yake asubuhi utaona maneno
ya nyimbo za Tenzi za Rohoni.Kama huamini pitia wall yake.
Huyu kwangu nampa namba mbili kama mtu anaepata Comments nyingi katika Wall yake.
Rose Mushi.
Dada
huyu napenda kumuita mpiganaji na mwanaharakati katika tasnia ya
Uwalimu katika kufundisha vijana na hata maswala mbalimbali katika
jamii.Ni Dada aliejaliwa busara na hekima katika kupambanua mambo na
kwenda na wakati na majira ya sasa.
Nathubutu
kusema atakuwa mwana Dada namba moja kwa wadada wanaopata Comments
nyingi katika Facebook lakini kwa mimi nampa namba tatu.
Hii ni sehemu ya moja ya jambo alilo andika katika Wall yake kwenye Facebook.
Poul Mashauri.
Kama
ni mafanyikio kwa Kaka huyu basi sasa amepiga hatua kubwa,kwa sasa
anakampuni kubwa yenye jina la East Africa Bureau Speakers na amekuwa na watu wengi wanaopitia kwenye Wall yake nakuangali
nini amesema.Pamoja na ubize aliokuwanao haiwezi kupita siku asiandike
jambo lolote katika Wall yake.
Wakati mwingine watu wanaweza wasi Comment lakini waka "like" kile alicho andika.Kwangu nampa namba tano.
0 comments: