Thursday, April 12, 2012

KANISA LA EFATHA MWENGE WAPINGA POLISI KUKAMATA WAUMINI WAKE.

By Jimmy  |  3:06 PM No comments

Kanisa la Efatha mwenge jijini Dar es salaam.

Taharifa na Gazeti la Mwanachi.

Kanisa la Efatha Foundation lililopo Mwenge, Dar es Salaam, limelalamikia kitendo cha Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuvamia na kuwakamata waumini wake 53 waliokuwa wakihudhuria ibada Jumatatu ya Pasaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kulikuwa na vurugu zilizosababishwa na waumini wa kanisa hilo waliokutwa na mapanga, nondo na sime kwa lengo la kubomoa majengo ya Kampuni ya Uchapaji ya Afro Plus, jambo ambalo liliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia.

Efatha Foundation na Afro Plus wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu, kila mmoja akidai kuwa mmiliki halali wa eneo hilo na suala lao lipo mahakamani.

Kenyela alisema polisi ilipokea taarifa za kuwapo moto katika Kiwanda cha Afro Plus, askari wake na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji walifika eneo la tukio, lakini walizuiwa na walinzi wa Efatha kuuzima.

Hata hivyo, watumishi wa kanisa hilo linaloongozwa na Mtume na Nabii Josephat Mwingira, jana walikanusha madai ya polisi na kwamba, polisi ndiyo walivamia waumini wake waliokuwa kwenye ibada.

“Jumatatu ya Pasaka saa 12:00 asubuhi, waumini wa Efatha walikuwa katika ibada ya Morning glory, ghafla walivamiwa kutoka nje na watu ambao baadaye walitambuliwa kuwa ni polisi,” alisema Natu Shilla, Katibu Mkuu wa Ephata Foundation.
Shilla alisema kutokana na kitendo hicho ibada ilisimama hasa baada ya mabomu ya machozi na risasi za moto kupigwa kanisani humo.

“Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia na polisi wakiwapiga kwa virungu na vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ukatapakaa damu,” alisema Shilla.

Shilla alikiri kukamatwa kwa waumini 53 na kwamba, kulikuwa na idadi ya waumini na wachungaji kati ya 60 na 70 na kuongeza kuwa, magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya kanisa yalivutwa.

“Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwa makusudi ili litekelezwe Kanisa la Efatha. Hii inatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa kwa huduma ya Efatha,” alisema Shilla.

Naye Godson Mmari ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo, alisema vurugu zilianzia kiwanja namba 90, baada ya polisi kuvamia wakidai kuwa kulikuwa na moto unaowaka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Efatha, Gothalm Mbele, alikiri walinzi wa eneo hilo kujibishana risasi na polisi kwa sababu walikuwa wakilinda fedha.

“Benki ni eneo nyeti linalohifadhi fedha za wananchi, kwa hiyo walinzi walihisi wamevamiwa na watu waliotaka kuhatarisha usalama wa fedha,” alisema Mbele.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP