Jengo Jipya la KKKT Kijitonyama.
Dk. Alex Malasusa,Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania akiwa katika ibada ya kuwekwa wakfu jengo la kitega uchumi lililojengwa na kanisa hilo usharika wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, jana.Dr Alex alikiri kuchukizwa kwake na baadhi ya makundi yanayotaka kulazimisha mambo ya hovyo yakiwemo ya kishoga kuingizwa katika Katiba.
Mbali na hilo, alikemea vikali tabia zinazofanywa na baadhi ya viongozi walioshindwa kusimamia rasilimali kwa maslahi ya nchi, badala yake wamejimilikisha wao.
Alisema kutokana na ubadhirifu huo, vijana wengi wamekosa ajira na kukiri kuwa ni jambo lililochangiwa na upendeleo katika baadhi ya taasisi.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Federick Sumaye, Anna Mkapa pamoja na wengine.
Mbali na jengo hilo lililogharimu sh bilioni 3.5, Malasusa alibariki nyumba iliyonunuliwa na kanisa hilo yenye thamani ya sh milioni 500 kwa ajili ya kuendesha shughuli mahsusi za kanisa.
Source-Sam sasali..
0 comments: