Thursday, September 15, 2011

KESHO KATIKA POWER DRIVE YA PRAISE POWER RADIO {NANI NI NANI} Ni Madam Ruti na Happy Kamili

By Jimmy  |  10:50 AM No comments

Kesho katika Power Drive tunakutana katika Nani ni Nani kuanzia 16:00-18:00 jioni,ambapo wewe kama Msikilizaji wetu unapiga Simu nakuchagu nani mkali kwako.Namba ya kutuma ujumbe mfupi wa Sms ni 0782-992123.

Happy Kamili akiwa kikazi zaidi.
Happy Kamili alianza Mziki Mwaka 1998.Lakini katika Mwaka huwo akuweza fanya vizuri sana,Ndipo alipo rudi tena Mwaka 2003 nakutoka na Albamu ya {Vuka Daraja}aikuishiapo Mwaka 2005 akaja na Albamu ya {Mshahara wa Dhambi ni Mauti}Albamu hii ilifanya vizuri nchini Kenya nakumpa mialiko sehemu mbalimbali Kenya,Uganda,na Mombasa.

Mwaka 2008 akaja na Albamu ya {Mpango wa Mungu lazima utimie}Albamu hii imemtangaza vizuri sana kuliko Albamu zote alizowaifanya.Mpango wa Mungu ameifanya katika Studio ya Kameta,nakatika Albamu hiyo nyimbo zilizo mtangaza ni Uwezi Mwenyewe,Usifiwe,Nitendee n.k

Happy Kamili ni Mama mwenye watoto (2) makazi yake ni mkoani Mbea.Kwa sasa Albamu yake inapatikana Madukani kote.Piga Kura yako sasa kupitia 0782-992123.

Madam Ruti Benson Mwamfupe.
Ni Mama wa watoto wawili,Kazi ya mziki wa injili alianza Mwaka 2006 akiwa na Kwaya ya Glory Temple Tabata Nchini ya Mchungaji Mwaipyana.

Mwaka 2009 alianza kufanya mziki akiwa kama yeye mwenyewe.Ali fanya nyimbo nyingi lakini akuzipeleka hewani,Kwani wakati huwo alikuwa akifanya kama majaribio.Mwaka 2010 alifunga mkanda nakujipanga kwajili yakwenda Nchini Kenya ku-record Mziki

Mwaka 2011 mwezi wa 3 tare 25 Madam Ruti alitua Nchini Kenya nakufanya Mziki chini ya Prdz-Geophrey Abass a.k.a PG.
Jina la Studio hiyo ni House of Grace ambapo waimbaji wengi wa Mziki wa injili ufanyaga kazi apo.
Ali-record Albamu nzima ambayo inakwenda kwajina la {AMENIBAMBA YESU}.Kwa mujibu wa Ruti Albamu hii kwa Sasa ipo sokoni Maduka yote ya mjini.

Nyimbo zilizo Mtangaza nikama Amenibamba Yesu,Inapendeza,Nitakutukuza Jehova n.k.Mpigie kura yako sasa Madam Ruti kupitia 0782-992123.




Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP