Kanisa la Tanzania Assemblies of God Jimbo la Zanzibar litaendelea kuhubiri kweli iliyopo kwenye Biblia ambayo ni maagizo ya Mungu.Hayo yalisemwa na Askofu wa Tanzania Assemblies of God Jimbo la Zanzibar Dickoson Kaganga kwenye majumuisho ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya kanisa katika section ya Magharibi.Ziara hiyo iliyoanza jumanne ilihitimishwa jana jioni katika ibada ya pamoja iliyofanyika kanisa la Tanzania Assemblies of God City Christian centre Kariakoo Zanzibar ambapo yeye Askofu ni mchungaji kiongozi.
Kabla ya kukaribishwa kwa Askofu mwangalizi wa kanisa section ya Magharibi aliwataka wachungaji kuwafundisha waumini wao juu ya misingi mikuu ya Assemblies of God, nae Mchungaji wa Mbweni ambaye ni katibu wa Jimbo la Zanzibar aliwataka waumini kuwa na msimamo na kuwa tayari kupata mafunzo mbalimbali ya kanisa ambayo yataimarisha Imani zao.Kwa upande mwingine Askofu Kaganga aliwataka waumini wajue TAG sio mali ya mtu wala kikundi cha watu bali ni taasisi ambayo inasimamia maandiko matakatifu na sio mataka ya mtu alisema "kanisa la TAG sio mali ya Kaganga au Dr Mtokambali" pia aliwataka wawe na msimamo na wayajue vizuri maandiko ili wasiyumbishe na upepo.Alisisitiza kuwa wataendelea kuwaambia kweli waumini wao kuwa uzinzi ni dhambi,wizi ni dhambi huku akisema lengo kuu ni kuponya roho za watu na sio jambo lolote zaidi.Alisema huwezi kuona na kuacha na kuoa na kuacha tu sivyo Biblia haisemi hivyo tutasimaia kweli hii na tutawambia kweli hii washirika wetu.
Ibada hiyo ilihitimishwa na harambee ya kuchangia ujenzi wa madirisha ya kanisa la Fuoni ambapo zaidi ya Tshs 300000/- zilipatikana na Askofu Kaganga aliahidi kuwa kama kutakuwa na upungufu wowote kanisa analosimamia litamalizia hicho kiwango.Ibada pia ilimalizika kwa maombi na maombezi. 

Askofu Dicskon Kaganga akiiyanza ibada
Mwangalizi wa TAG Section ya Magharibi akieleza jambo
Askofu Dickson Kaganga akiteta jambo na washekina.
Mchungaji Msaidizi Solomoni Mwale akihudumu.
Askofu Kaganga na Mchungaji Marwa wa Mbweni wakihimiza kusimamia maandiko.
Shekina wakiimba mwisho wa ibada...
Na ripota wa Unclejimmytemu.com Stewart Njelekela ( IT Team CCC Kariakoo Zanzibar)
0 comments: