Kufatia fukufuku la miss Tanzania ambalo linaendelea kwa miss 'Sitti Mtemvu' kufoji umri wa miaka yake katika shindano la miss Tanzaania lililofanyika wiki tatu zilizopita limeleta maneno mengi kwa wapenzi wa shindano hilo.Kufatia kitendo hiko mitandao ya kijami vyombo vya habari kama magazeti na TV vimekua vikilaani kitendo hiko ambacho kinaonekana kama kulifanyika mchezo mchafu kwa kamati ya miss Tanzania.
Wakati fukufuku hili la miss Tanzania likiwa bado la moto kila mtu akisubiri hatima yake,Mchungaji Maboya hivi karibuni alikua kwenye mkutano wa nje kwa wiki mbili mkoani Morogoro wilaya ya Ifakara ambapo katika mahubiri yake aligusia uhusiano wa Uzuri na Pesa na kumuhusisha kwa kumtaja alwatani Miss Tanzania SITTI MTEMVU
Kwa hisani ya Unclejimmytemu.com msikilize hapo chini Mchungaji Maboya akieleza uhusiano wa fedha na uzuri mdau wangu.
0 comments: