Usiku wa jana katika Club ya Sansiro Sinza kulifanyika mashindano ya Serengeti Super Nyota Diva yanayo ratibiwa na Clouds fm chini ya DJ Fetty.
Hellen alionyesha uwezo wake toka mwanzo wa shindano hilo.....aliingia fainali na mwanadada Emmy Wimbo na kumwaga kwa kura nyingi na mpaka kuwapa shida majaji wa shindano hilo,ambao walikua Barnaba Elias,Producer Tudd Thomas na Dj Fetty.Mpaka mwisho wa shindano Hellen aliibuka mshindi
Mshindi wa Dar es salaam ataungana na washindi waliopatikana mikoani na kufanya fainali moja itakayompata mshindi mmoja.
Mshindi atakayepatikana atafanya kolabo na Diamond kwa kurecord naye nyimbo 3 pamoja na kupewa shilingi milioni 1 mkononi
Mshindi atakayepatikana atafanya kolabo na Diamond kwa kurecord naye nyimbo 3 pamoja na kupewa shilingi milioni 1 mkononi
Unclejimmytemu.com baada ya shindano hilo kumalizika ilitaka kuthibitisha kama kweli Hellen George ni mshirika wa Word Alive Centre na Kanisa linasemaje juu ya yeye kushiriki kwake mashindano hayo.
Unclejimmytemu.com ilifanya maongezi na kiongozi mmoja wa Kanisa na kuambiwa Hellen kwa sasa siyo mshirika wala muimbaji wa Word Alive hivyo hawatambui ushiriki wake na hawajui halipo.
Baada ya kutajwa mshindi Hellen George akitokwa na machozi
Hapa walipoingia Tatu bora kabla ya Hellen kuibuka mshindi.
0 comments: