Mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika
Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ anapigiwa debe kwa kiasi kikubwa
kusindikiza uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa-The Sound of Worship ya John
Lissu.
Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa
kufanyika Oktoba 5 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,
ambapo
waimbaji mbalimbali watakuwepo.
Akizungumza na gazeti hili, Lissu
alisema amekuwa akipokea maombi kutoka kwa mashabiki mbalimbali wakimuomba afanye
kila njia kuhakikisha Mahlangu anakuwepo kwenye uzinduzi huo.
Msama alipokua akiongea na vyombo vya habari kuhusu Tamasha la John Lisu.
“Maandalizi ya uzinduzi yanenda vizuri,
naamini mashabiki wangu watafurahi sana, wamekuwa wakinipigia simu kuomba
wasanii wengi, lakini Mahlangu anaomba sana ahudhurie uzinduzi wangu, ” alisema
Lissu.
Mahlangu ni muimbaji ambaye
anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika ambaye pia anamudu kuimba
Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.
Mbali ya kuwa maarufu katika
nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji ambaye ana uwezo wa
kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo ni Word Praise Christian
Centre Intenational lililoko Tembisa.
Albamu ya Lissu ambaye ana sifa ya
kupiga muziki wa live ina nyimbo 18 zilizogawanywa katika maeneo mawili, ambazo
ni Wakusifiwa, Wastahili Sifa, Mataifa ya Kujua, Inuka, Uko Hapa, Nijaze,
Nitaongozwa, Wastahili Bwana, Roho Mtakatifu, Mtakatifu na Umeinuliwa.
Nyingine ni Yu Hai Jehova, Atikisa,
Nijaze, Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho, Haleluya na
Mungu Ibariki.
Chanzo cha habari-Dira


0 comments: