Mara zote nimekua nikipiga kelele juu ya ubora wa video na namna ya kuupenyeza muziki wetu wa Gospel East Africa na duniani.Wengi wamekua waki nisema lakini sita acha kupaza sauti hadi pale watakapo hamua kukubali kuwekeza katika muziki wetu wa Gospel.Hii inatoka na wenzetu wa muziki wa Bongo flava kuwekeza hela nyingi katika kazi zao hasa utengenezaji wa video zao.Angel Bernad atakuwa mwanamuziki wa kwanza kwenye gospel kuamua kuwekeza na kufaya video yenye ubora mkubwa na Director wa video kutoka Kenya anayejulikaa kwa jina la Kevin Bosco,director ambaye amefanya kazi na wasanii mbalimbali wakiwemo Ambwene Yessaya(AY) kwenye video ya Asante,Victoria Kimani Prokoto na wengine wengi.Utengenezaji wa video hii ya I NEED TO RAIN umegharimu shilingi milioni
tano za kitanzania,ngoja tuisubiri hadi hapo itakapotoka mdau wangu.BIG UP ANGEL




0 comments: