Thursday, June 12, 2014

MUENDELEZO WA MAISHA YA BAHATI BUKUKU

By Jimmy  |  11:39 AM No comments

Japokuwa nimejitahidi sana kuisahau siku hii lakini moyo wangu umeshindwa kufanya hivyo. Kila ninapotulia, iwe sebuleni au chumbani kwangu, picha ya siku hiyo huwa inanijia kichwani mwangu. Tukio hilo limekuwa kubwa kwangu huku likiendelea kujirudia kama mkanda wa filamu.
Nilipenda kwenda shule kusoma, na hii ilikuwa njia mojawapo ya kuepuka kufanya kazi za nyumbani, hasa kuosha vyombo kitu nilichokuwa nikikichukia mno.
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini mama alijitahidi sana kuniweka katika mazingira ambayo mtoto wa kike anatakiwa kuwa.
Achukia kuosha vyombo
Kila siku alikuwa akinitaka nioshe vyombo, hii ilikuwa kazi pekee niliyokuwa nikiichukia mno. Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, mama alikuwa akinipa maziwa na kiporo cha jana, nikimaliza kula, alikuwa akiniambia nioshe vyombo nilivyovitumia.
Nilikereka mno lakini sikuwa na jinsi, nilibaki nikilalamikalalamika lakini mwisho wa siku niliosha vyombo mbele yake huku akionekana kuwa na furaha.

AWA KIONGOZI WA KUIMBA
Ijulikane kwamba kuimba ni kipaji nilichozaliwa nacho. Nakumbuka kipindi hicho mimi ndiye nilikuwa kiongozi wa nyimbo mbalimbali tulizokuwa tukiimba shuleni. Sauti yangu haikuwa nzuri, ilikuwa ni ya kukoroma sana lakini kila nilipokuwa nikiimba walimu waliipenda na ilikuwa ni lazima ujue kwamba ‘huyo anayeimba ni Lusako’.
AANZA DARASA LA KWANZA
Baada ya kusoma shule ya chekechea kwa miaka miwili, mwaka 1990 nilitakiwa kwenda kuanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Muungano ambayo haikuwa mbali kutoka tulipokuwa tukiishi.
Kama kawaida yangu, siku hiyo niliamka asubuhi sana huku nikiwa na hamu ya kuanza darasa la kwanza. Moyo wangu haukuweza kusahau, bado niliendelea kukumbuka miaka miwili iliyopita ambapo nilishindwa kulishika sikio langu la upande wa kushoto kwa kutumia mkono wangu wa kulia kwa kuupitisha kichwani.
Kwanza kabla ya yote, hapohapo nyumbani, nikajaribu kulishika sikio langu, nikafanikiw
a.
ACHEKELEA KUJIUNGA NA SHULE YA MSINGI
Naweza kusema kwamba katika mwaka huo, siku hiyo ndiyo nilikuwa na furaha kupita kawaida. Nilipenda sana shule, kila nilipokuwa nikiwaona wanafunzi wakipita nyumbani huku wakiwa wamevalia sare zao za shule, niliona wivu moyoni.
Leo hii na mimi nilitakiwa kwenda kuanza darasa la kwanza! Asubuhi ya siku hiyo, mama akaniletea sketi na shati huku chini nikivalia soksi za pundamilia.
Sikuwa na sare za shule hivyo siku hiyo nilivalia nguo za nyumbani ila miguuni nilikuwa na soksi hizo za pundamilia. Baada ya kutembea kwa umbali mdogo, nikaelekea shuleni huku nikiongozana na baba, mzee Bukuku.
Watoto waliokuja kuanza shule walikuwa wengi na zoezi lilikuwa lilelile la miaka yote, kushika sikio lako. Wapo walioshindwa ambao walilia kama nilivyofanya miaka miwili iliyopita lakini pia walikuwepo wale waliofaulu na kutakiwa kujiunga na shule hiyo kwa ajili ya kuanza na elimu ya msingi huku nikiwa nimeandikishwa jina jingine na kuitwa Bahati.
                              ***
AANZA MASOMO
Niliipenda masomo, niliipenda shule kwa jinsi majengo yake yalivyokuwa. Yalipendeza na kuvutia sana. Siku hiyohiyo ambayo baba alikuwa amenipeleka shuleni hapo, tukaingizwa darasani na kupangwa, siku iliyofuata, tukaanza masomo huku tukiwa watoto zaidi ya arobaini katika darasa moja.
Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kama nilivyokuwa. Hakukuwa na utulivu, kila wakati wanafunzi walikuwa wakipiga kelele, nadhani kwa walimu au kwa watu waliokuwa katika mitaa yenye watoto wengi watakuwa wanalitambua hili, jinsi watoto wanavyopiga kelele zenye kuleta kero.
AONGOZA KWA UTUNDU
Kati ya wanafunzi wote waliokuwa darasani, mimi ndiye nilionekana kuwa mtundu. Kwanza sikutulia sehemu moja, nilionekana kama mtu aliyekuwa akitafuta kitu fulani, muda huu unaweza kuniona hapa na baadaye kuniona kule.
UTUNDU WAMPA UMONITA
Kutokana na utundu wangu wa muda mfupi, hata mwalimu wa darasa hilo aitwaye Rugemilila alipoingia darasani, akanichagua niwe ‘monita’ yaani kiongozi wa darasa lile.
Maisha ya nyumbani yaliendelea kuwa vilevile kwamba kila nilipokuwa nikirudi na kula chakula, mama alinitaka nioshe vyombo. Bado mama alinifundisha mambo mengi huku akitamani sana niwe kama wasichana wengine, nadhani mbele ya maisha yangu aliyaona  kwani kwa kile alichokuwa akikitaka ndicho kimeweza kunisaidia sana kipindi hiki.
AKAMUA NG’OMBE MAZIWA 
Kazi zote za nyumbani ambazo alikuwa akizifanya mama, ilikuwa ni lazima na mimi nizifanye. Siku ambayo sikuwa nikienda shule, ilikuwa ni lazima nipike japo chai na kufanya usafi nyumbani hapo huku nikisaidiana naye.
Nyumbani kulikuwa na ng’ombe, kila siku, hata kabla ya kwenda shule ilikuwa ni lazima niamke asubuhi sana, nikamue maziwa na kisha mtu ambaye alikuwa akihusika kwa ajili ya kwenda kuwachunga akiwatoa zizini na kwenda nao machungoni.
ACHUNGA NG’OMBE
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu ya kila siku. Siku ambazo sikuwa nikielekea shuleni, pia nilikuwa nikichukuliwa na kupelekwa machungoni. Nilichukia kazi nyingine lakini hii ya kuwapeleka ng’ombe machungoni niliipenda kwa sababu ilinipa nafasi ya kuondoka nyumbani hapo kwenda kuzurura na ng’ombe hao.
AUZA CHIPSI
Kutokana na utundu niliokuwa nao na ujanja wa hapa na pale, mwalimu wangu wa darasa akanichagua niuze chipsi zake. Wanafunzi wengi walikuwa wakiitamani kazi hii kwani walijua fika kwamba mara unapouza na nyingine kubaki, walimu huwa na kawaida ya kukupa mfuko mmoja ule.
globalpublishers.info

Nilipenda kwenda shule kusoma, na hii ilikuwa njia mojawapo ya kuepuka kufanya kazi za nyumbani, hasa kuosha vyombo kitu nilichokuwa nikikichukia mno.
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini mama alijitahidi sana kuniweka katika mazingira ambayo mtoto wa kike anatakiwa kuwa.
Achukia kuosha vyombo
Kila siku alikuwa akinitaka nioshe vyombo, hii ilikuwa kazi pekee niliyokuwa nikiichukia mno. Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, mama alikuwa akinipa maziwa na kiporo cha jana, nikimaliza kula, alikuwa akiniambia nioshe vyombo nilivyovitumia.
Nilikereka mno lakini sikuwa na jinsi, nilibaki nikilalamikalalamika lakini mwisho wa siku niliosha vyombo mbele yake huku akionekana kuwa na furaha.
AWA KIONGOZI WA KUIMBA
Ijulikane kwamba kuimba ni kipaji nilichozaliwa nacho. Nakumbuka kipindi hicho mimi ndiye nilikuwa kiongozi wa nyimbo mbalimbali tulizokuwa tukiimba shuleni. Sauti yangu haikuwa nzuri, ilikuwa ni ya kukoroma sana lakini kila nilipokuwa nikiimba walimu waliipenda na ilikuwa ni lazima ujue kwamba ‘huyo anayeimba ni Lusako’.
AANZA DARASA LA KWANZA
Baada ya kusoma shule ya chekechea kwa miaka miwili, mwaka 1990 nilitakiwa kwenda kuanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Muungano ambayo haikuwa mbali kutoka tulipokuwa tukiishi.
Kama kawaida yangu, siku hiyo niliamka asubuhi sana huku nikiwa na hamu ya kuanza darasa la kwanza. Moyo wangu haukuweza kusahau, bado niliendelea kukumbuka miaka miwili iliyopita ambapo nilishindwa kulishika sikio langu la upande wa kushoto kwa kutumia mkono wangu wa kulia kwa kuupitisha kichwani.
Kwanza kabla ya yote, hapohapo nyumbani, nikajaribu kulishika sikio langu, nikafanikiwa.
ACHEKELEA KUJIUNGA NA SHULE YA MSINGI
Naweza kusema kwamba katika mwaka huo, siku hiyo ndiyo nilikuwa na furaha kupita kawaida. Nilipenda sana shule, kila nilipokuwa nikiwaona wanafunzi wakipita nyumbani huku wakiwa wamevalia sare zao za shule, niliona wivu moyoni.
Leo hii na mimi nilitakiwa kwenda kuanza darasa la kwanza! Asubuhi ya siku hiyo, mama akaniletea sketi na shati huku chini nikivalia soksi za pundamilia.
Sikuwa na sare za shule hivyo siku hiyo nilivalia nguo za nyumbani ila miguuni nilikuwa na soksi hizo za pundamilia. Baada ya kutembea kwa umbali mdogo, nikaelekea shuleni huku nikiongozana na baba, mzee Bukuku.
Watoto waliokuja kuanza shule walikuwa wengi na zoezi lilikuwa lilelile la miaka yote, kushika sikio lako. Wapo walioshindwa ambao walilia kama nilivyofanya miaka miwili iliyopita lakini pia walikuwepo wale waliofaulu na kutakiwa kujiunga na shule hiyo kwa ajili ya kuanza na elimu ya msingi huku nikiwa nimeandikishwa jina jingine na kuitwa Bahati.                              AANZA MASOMO
Niliipenda masomo, niliipenda shule kwa jinsi majengo yake yalivyokuwa. Yalipendeza na kuvutia sana. Siku hiyohiyo ambayo baba alikuwa amenipeleka shuleni hapo, tukaingizwa darasani na kupangwa, siku iliyofuata, tukaanza masomo huku tukiwa watoto zaidi ya arobaini katika darasa moja.
Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kama nilivyokuwa. Hakukuwa na utulivu, kila wakati wanafunzi walikuwa wakipiga kelele, nadhani kwa walimu au kwa watu waliokuwa katika mitaa yenye watoto wengi watakuwa wanalitambua hili, jinsi watoto wanavyopiga kelele zenye kuleta kero.
AONGOZA KWA UTUNDU
Kati ya wanafunzi wote waliokuwa darasani, mimi ndiye nilionekana kuwa mtundu. Kwanza sikutulia sehemu moja, nilionekana kama mtu aliyekuwa akitafuta kitu fulani, muda huu unaweza kuniona hapa na baadaye kuniona kule.
UTUNDU WAMPA UMONITA
Kutokana na utundu wangu wa muda mfupi, hata mwalimu wa darasa hilo aitwaye Rugemilila alipoingia darasani, akanichagua niwe ‘monita’ yaani kiongozi wa darasa lile.
Maisha ya nyumbani yaliendelea kuwa vilevile kwamba kila nilipokuwa nikirudi na kula chakula, mama alinitaka nioshe vyombo. Bado mama alinifundisha mambo mengi huku akitamani sana niwe kama wasichana wengine, nadhani mbele ya maisha yangu aliyaona  kwani kwa kile alichokuwa akikitaka ndicho kimeweza kunisaidia sana kipindi hiki.
AKAMUA NG’OMBE MAZIWA 
Kazi zote za nyumbani ambazo alikuwa akizifanya mama, ilikuwa ni lazima na mimi nizifanye. Siku ambayo sikuwa nikienda shule, ilikuwa ni lazima nipike japo chai na kufanya usafi nyumbani hapo huku nikisaidiana naye.
Nyumbani kulikuwa na ng’ombe, kila siku, hata kabla ya kwenda shule ilikuwa ni lazima niamke asubuhi sana, nikamue maziwa na kisha mtu ambaye alikuwa akihusika kwa ajili ya kwenda kuwachunga akiwatoa zizini na kwenda nao machungoni.
ACHUNGA NG’OMBE
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu ya kila siku. Siku ambazo sikuwa nikielekea shuleni, pia nilikuwa nikichukuliwa na kupelekwa machungoni. Nilichukia kazi nyingine lakini hii ya kuwapeleka ng’ombe machungoni niliipenda kwa sababu ilinipa nafasi ya kuondoka nyumbani hapo kwenda kuzurura na ng’ombe hao.
AUZA CHIPSI
Kutokana na utundu niliokuwa nao na ujanja wa hapa na pale, mwalimu wangu wa darasa akanichagua niuze chipsi zake. Wanafunzi wengi walikuwa wakiitamani kazi hii kwani walijua fika kwamba mara unapouza na nyingine kubaki, walimu huwa na kawaida ya kukupa mfuko mmoja ule.
Chazo cha habari-globalpublishers.info

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP