maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency
Mamlaka
inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli na ina
lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania.
Mamlaka
ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo
husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio,
televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).
Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali
mbaya ya hewa zinatolewa na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji
taarifa maalum za kiofisi (official weather statement).
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua
zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya
habari, mtandao wa kijamii wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.
Tunawatakia
shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
0 comments: