MTU (Mwanga wa Tumaini) ni asasi chini ya uangalizi wa na
kanisa la Dar es Salaam PentecostalChurch (DPC ) lililopo kinondoni Dar es
Salaam ambayo inahusika na kusaidia wenye uhitaji . Lengokubwa la asasi hiyo ni
kutoa misaada mbali mbali ikiwemo huduma ya matibabu na dawa bure,
ushaurinasaha pamoja na ushauri wa kisheria kwa wale wanaohitaji. Vile vile
wanatoa huduma ya kupima VVUna ushauri nasaha wakishirikiana na PASADA. Misaada
ya kijamii kama vile mavazi na chakula hutolewabure kama sehemu ya huduma ya
asasi ya MTU. MTU imekua ikitoa huduma hizi maeneo ya Kinondoni,ila mipango ipo
ya kupanua wigo wa huduma.
Leo tarehe 3 Mei 2014, MTU wapo viwanja
vya shule ya msingi Hananasifu Kinondoni wanatoa huduma hi .Katika huduma zinazo fakia wanachi leo ni pamoja na huduma za kitabibu, huduma za kisheria,na ushauri nasaha.
MTU imeshirikiana na kanisa la DPC katika kuandaa tukio la
leo.
Ana Bela na Pastor Safari eneo la tukio
Mtunishi akifanya maombezi kwa mgeni aliyefika eneo la tukio
Wakazi mbalimbali wa maeneo ya Kinondoni
0 comments: