Huduma ya Spirit Word Ministry chini ya Pastor Ceasar Masisi siku ya jana ilianda chakula cha kiroho kwaajili ya kutoa mafundisho yenye kulenga mtazamo mpya katika kizazi hiki cha 2014.Mafundisho hayo yalifanyika siku ya J/pili majira ya saa nane mchana katika
Hotel ya Wanyama iliyopo Sinza mori ambapo wageni mbalimbali walikuwepo akiwemo Askofu Edga Mwamfupe,Pastor Huruma,Stara Thomas,Madam Ruth,Christina Matai,Robert Bukerebe,Mchungaji Elizabeth wa Grace Product na Momoza ya Clouds TV.
Huduma hii itakuwepo kila J/pili Sinza Mori (Wanyama Hotel),nia na madhumini ni kujifunza neno la Mungu hivyo wanakaribisha watu wote dini yoyote.Muda ni saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni.
0 comments: