Mihula mitatu ya maisha ya mwanadamu:
Nimechagua
kuiwasilisha mihula mitatu kwa kutumia taswira hii ifuatayo ambayo tutakuwa
tukiirejea kila mara kwa kadiri tunavyoendelea kujifunza juu ya dhana ya
kufanya maamuzi hasa kwa mwanga wa maneno ya Mungu kwa kinywa cha nabii Yoeli
HAPA
NDIYO KWENYE BONDE LA KUKATA MANENO.
|
i. Maisha kabla ya kuzaliwa
Luka 1:30-33
“Malaika
akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama,
utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo
atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi
cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake
utakuwa hauna mwisho.”
Mathayo 1:21
“Naye atazaa
mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake
na dhambi zao.”
Ni jambo gani linakuijia mawazoni usomapo mistari
hiyo?... Hata mimi kwa muda nilikuwa ninaona mafundisho ya Krsimasi kila
nisomapo mpaka nilipofunuliwa jambo hili kwa namna ya tofauti. Hawa watakatifu
wawili, waandishi wa Injili, wanaleta picha ya namna ya kipeke sana katika
habari ya kuzaliwa kwa Yesu. Hebu wacha nikuonyeshe kitu hapa… Kama umesoma
vizuri na kwa umakini katika mistari hiyo utagundua ya kwamba imeandikwa kabla
Yesu Kristo hajazaliwa. Mtakatifu Luka ameandika habari kabla hata ya mimba ndani
ya Mariamu; na Mathayo ametueleza habari hiyo wakati wa mimba – lakini yote kwa
yote ni kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Kitu gani unaona? Malaika anazungumza na
Mariamu na kutaja jinsi ya mtoto kuwa atakuwa mwanaume, anataja jina la mtoto
kwamba ataitwa Yesu na anataja baadhi ya majukumu yake baada ya kuzaliwa, yaani
wakati wa kuishi kwake. Hebu tazama kitu anachotuonyesha Mathayo, malaika
anamtokea Yusufu ndotoni na kumpa habari kwa upana wake na katika habari hizo
malaika anataja jina la mtoto na anataja kusudi la kuja kwake ulimwenguni. Yote
hayo yanatajwa kabla ya mtoto kuzaliwa, yaani kabla hajaanza kuishi na kutembea
ulimwenguni tayari ameshajulikana kwa namna kubwa sana, taarifa zake
zinajulikana, jina lake, jinsi yake na kusudi la kuwepo kwake linajulikana.
Wengi hudhani kwakuwa ni Yesu, mwana wa Mungu,
hivyo kwake ilipaswa kuwa dhahiri- ilikuwa ni ya kipekee (special case). Kabla
hujahitimisha hivyo ni vyema ukumbuke kuwa Yesu alikuwa mwanadamu asilimia mia
moja na Mungu asilimia mia moja, kwahiyo tunapozungumzia sehemu yake ya
uanadamu ni vyema tukatazama kwa jicho hilo tu… Si unajua kuzaliwa ni sehemu ya
uanadamu?
0 comments: