Wakati tukio
la Bomu kulipuka ndani ya kanisa la Kiinjili kilutheri Tanzania,(KKKT) Usharika
wa Imani Makongoro,jijini Mwanza likiwa halijasahaulika akilini mwa watu,Kanisa
moja jingine la EAGT wilayani Mafia mkoani Pwani limeteketezwa kwa Moto.
Katika
Kipindi cha miaka miwili sasa takribani makanisa 10, yameteketezwa kwa Moto
nchini Tanzania ambapo matano kati ya hayo yakichomwa mwaka juzi katika mkoa wa
Dar es Salaam kufuatia kitendo cha mtoto wa miaka 13 kukojolea kitabu cha imani
ya waislam Quran huku mengine yakichomwa katika mikoa ya Kigoma,Morogoro, na
Zanzibar.
Tofauti
na uchomaji Moto,pia makanisa kadhaa hapa nchini yalilipuliwa kwa mabomu ya
kurushwa na kutegeshwa kama tukio la hivi karibuni katika jiji la Mwanza.
Tukio lingine la shambulio la Bomu kanisani lilitokea mwaka jana jijini Arusha ambapo kanisa moja la katoliki lilishambuliwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono tena wakati washirika wake wakiwa ibadani na kujeruhi takribani watu 25.
Tukio lingine la shambulio la Bomu kanisani lilitokea mwaka jana jijini Arusha ambapo kanisa moja la katoliki lilishambuliwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono tena wakati washirika wake wakiwa ibadani na kujeruhi takribani watu 25.
Katika Kanisa la Mafia ambalo limechomwa moto hivi karibuni Katibu mkuu wa
kanisa la EAGT Taifa Mchungaji Brown Mwakipesile alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo lililotokea katika kanisa la Evangelistic Assemblies of God Miburani
lililoko katika kata ya Miburani wilayani Mafia.
Hata Hivyo Mwakipesile alisema asingeweza kulizungumzia kiundani suala
hilo kwa vile aliyekua na nafasi nzuri ya kulifafanua kiundani alikua
Askofu wa EAGT jimbo la mashariki na Pwani Nicodemus Nyenye ambaye hata hivyo
simu yake haikuweza kupatikana.
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo lililochomwa
moto Patience Ndunguru alipopigiwa simu kulitolea maelezo janga hilo pamoja na
kukiri alisema kua asingeweza kulizungumzia kwa vile alikua Ibadani hivyo
mwandishi ampigie baadae.mpaka tunakwenda mitamboni simu yake ilikua imefungwa,aidha kwa mujibu wa vyanzo vya habari uhalifu huo unatajwa kufanywa na watu wasiojulikana ijumaa ya Mei 2,2014 majira ya sasa tano usiku.
Vyanzo hivyo vimeeleza kua moto huo uliteketeza kila kitu vikiwemo vyombo vya kuhubiria na muziki,viti vya madhabahuni na vya waumini pam oja na paa zima lililoezekwa kwa mabati na kuta za jengo hilo zilizojengwa kwa matofali.
Thamani ya Uharibifu huo haikuweza kupatikana kwa mara moja na kwamba tukio hilo tayari linashughulikiwa na jeshi la polisi ambalo nalo halikuweza kupatikana kulitolea ufafanuzi.
Cha cha habari mjap inc....
0 comments: