Hesabu 13:25- 33
Ndugu msomaji
wangu tafadhali fuatilia kwa makini safu ya mtiririko wa baada ya kujifunza kwa
muda wa majuma kadhaa sasa leo ni fulsa nyingine ya ya kuangalia kiini cha somo
kwa mtiririko uliochambuliwa kutoka kwenye vyanzo mbali mbali kama
Biblia,vitabu na nyenzo nyinginezo(marudio yenye uchambuzi yakinifu)
Mara nyingi
maono/malengo huchukua muda mrefu mpaka kufikia katika hatua ya mchakato wa
matendo ambayo yataleta uhalisia wa
kitu husika, Lakini pamoja na matarajio, maono au malengo ya muda mrefu nataka tuone jinsi vile taarifa inavyoweza kubadili kwa haraka muono wako na kile ulichokitarajia. (Matokeo sahii huja kwa chanzo sahihi na taarifa sahihi...Matokeo mabaya huja kwa chanzo kibaya na taarifa mbaya)
kitu husika, Lakini pamoja na matarajio, maono au malengo ya muda mrefu nataka tuone jinsi vile taarifa inavyoweza kubadili kwa haraka muono wako na kile ulichokitarajia. (Matokeo sahii huja kwa chanzo sahihi na taarifa sahihi...Matokeo mabaya huja kwa chanzo kibaya na taarifa mbaya)
Hesabu 13:25- 33
13.25 Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku
arobaini.
13.26 Wakaenda
wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli,
katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote,
wakawaonyesha matunda ya nchi.
13.27 Wakamwambia
wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa
maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.
13.28 Lakini watu
wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa
sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.
13.29 Amaleki anakaa
katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima,
na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.
13.30 Kalebu
akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza
kushinda bila shaka.
13.31 Bali wale watu
waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa
maana wana nguvu kuliko sisi.
13.32 Wakawaletea
wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi
tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu
wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
13.33 Kisha, huko
tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona
nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Hii ni habari ya wana islael ambao walitoka misri kwa lengo/wazo
moja la kwenda kanaani kwenye nchi ya ahadi ambayo Mungu aliwaahidi ni habari
ndefu lakini lengo au mkazo wa somo letu uko kwenye mistari hiyo michache
tuliyosoma hapo juu.Mungu alimwambia musa atume wapelelezi kwenda kuichunguza
nchi ile sasa ukisoma hapo juu kuanzia huo mstari wa 25 utaelewa zaidi....
Ukisoma habari hiyo utagundua kutumwa kwa wale wapelelezi
lengo ilikua ni kuleta habari ambayo
ingekua msaada kwao ili wajue wanapaswa kuingiaje katika mji ule....Sasa lengo
kuu hapa ilikua ni habar,habari ya aina
yoyote ile itakayo wajia iwe nzuri au mbaya,ili kutimiza lengo la
kuifikia ile nchi ilikua ni lazima wasonge mbele. Lakini ukisoma kuanzia mstari
wa 28 utaona jinsi watoa taarifa (wapelelezi) walivyoanza kubadili mtazamo wa
watu kupitia taarifa yao mbaya iliyotokana na uchunguzi walioufanya.Ukiendelea
kusoma utaona walizidi kupamba maneno kiasi cha kusababisha umati wote kuamaki
na kukubaliana na maneno yao......Rejea mstari wa 31- 33.
Ilifika mahali wakajifaninisha na panzi, na ukiendelea kusoma
sura inayofuata utaona jinsi watu walivyoingiwa hofu na kuanza kulalamika
ilifika mahali Mungu akaghadhibika na katika umati wote ule wa watu waliokua na
ndoto za kuifikia nchi ya kaanani na kuimiliki ni watu wawili tu ndio ambao
walifanikiwa kuingia nchi ile. (Hesabu
14:22-24)
MUHIMU: Ukichukua wasaa na kusoma vizuri juu ya habari
hii utatambua kwamba watu hawa si kwamba walikurupuka kuanza safari ile..la
hasha! Hii ilikua ni ahadi na mpango kamili kabisa wa Mungu ambayo ulikuwepo
toka vizazi na vizazi na waliishi miaka yote wakiisubiri ahadi hiyo.Lakini
ghafla baada ya kusubiri ya kuhangaika kwa miaka mingi utaona hapa kuna kitu
kinatokea ambacho kinasababisha mambo kuharibika ghafla,Kitu hicho ni
TAARIFA.Haijalishi ni kwa muda mrefu kiasi gani umehangaika kufanya kitu au
umekua katika mchakato wa kungoja matokeo ya malengo yako,unapoiruhusu tu taarifa potofu iingie katika ufahamu wako jua
wazi inaweza ikaua juhudi na nguvu yote
uliyoitumia na ukapata hasara kwa haraka
ukilinganisha na muda ulioutumia katika mchakato wa kuyatengeneza
matokeo(KUBOMOA NI RAHISI KULIKO KUJENGA) Niliongea awali kwamba taarifa ni
taarifa tu haijalishi kwamba ni nzuri au mbaya maadam ni taarifa lazima
itaathiri maamuzi na matokeo yako.Pamoja na taarifa mbaya walioipokea watu hawa
walikua na uchaguzi wa kufanya kwasababu kuna watu ambao walileta taarifa nzuri
lakini waliipuuza na kuchagua kusikiliza na kuiamini taarifa mbaya na potofu
ambayo iliwagharimu sana............
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com

0 comments: