Amosi akiwa na mkewe baada ya kufunga harusi.
Mungu anaendelea kuonyesha uwezo wake wa kubadilisha maisha
ya wanadamu, zaidi upendo wake kwa wanadamu kuonyesha kuwa hana upendeleo hata
kama mtu ni mwovu namna gani basi yeye bado yeye anampenda tu, kwani yeye
hakuja kwa waliowazima maana hawahitaji dakitari bali wale waliopotea, walio
kwenye vifungo vya shetani na kuwahamishia katika pendo lake na kuwapa maisha
ya heshima yenye furaha na upendo. hii inamhusu sana aunt Asu ambaye hapo mwazo
alikuwa shoga
wa kutupwa ameshaolewa mara nyingi na kuachwa, na si hivyo tu
bali aliishi maisha ya kudhalilika ya kuvyaa mavazi ya kike na kujipodoa.
lakini upendo wake Mungu na neema ya kristo ikamwangazia na kupata neema hii ya
wokovu na kuamua kuokoka.Msajili wa ndoa hiyo mch D. Kanemba na mapaparazi nao walikuwepo
Kwa kweli Yesu anabadilisha kabisa na kumfanya mtu kuwa kiumbe kipya huyu sasa tena siyo Aunt Asu kama wengi walivyozoea kumwona sasa ni Mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa amejikita katika kumtumikia Mungu kwa sasa amesharekodi albamu yake ya nyimbo za injili, na amesha anza kurekodi na dvd muda si mrefu itaingia katika soko la muziki wa injili, kati ya nyimbo ameimba kuna unaoelezea maisha yake wakati anatumikishwa na shetani lakini sasa kabadilika.
Hili tukio la kihistoria lilifanyika katika kanisa la TAG
Magomeni tar 13-04-2014 Amosi alipofunga pingu za maisha na kudhihilishia uma
kuwa sasa yeye kabadilishwa na yesu na sasa ana maisha mapya.
0 comments: