SAFU
YA FRED MSUNGU: BADILI CHANZO CHA TAARIFA
JINSI
ULIVYO LEO NI MATOKEO YA ULICHOKISIKIA NA KUKIAMINI
SEHEMU YA NNE.....
I.
NINI
CHANZO SAHIHI NA NINI SI CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA
Jibu la swali
hili linategemea sana na maisha uliyochagua (hatma yako) na aina ya malengo
uliyonayo.Inawezekana sana chanzo hicho hicho kikawa ni sahihi sana kwa wengine
lakini kwako kisiwe ni sahihi,Naweza nikawa nimekupa wakati
mgumu wa kufikiri lakini kadri unavyozidi kusoma ndivyo fikra yako inapanuka na
ninaamini mpaka mwisho tutakua kwa pamoja tumeipata maana halisi ya somo hili.
MUHIMU: Jambo la
muhimu sana kujua hapa ni hili ‘ Huwezi kuja kuyafikia matokeo makubwa zaidi ya
fikra zako zinavyoona....Jinsi vile unawaza ,unaona juu yako na juu ya kesho (hatma)yako
ndivyo vile utakavyokua.Hakuna muujiza wala uchawi wa aina yeyote katika hili
,Kipimo au kiwango ulichonacho juu yako ndicho hicho
utakua milele.(Mithali 23:7 )Ajionavyo mtu nafsini mwake
ndivyo alivyo.
Ukiisoma hiyo
mithali utaona hapo ametumia neno ‘Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo’
Naliangalia kwa jicho la tofauti sana neno NDIVYO ALIVYO!Maana ninayoipata hapa
ni kwamba kile unachokiona ndani yako haijalishi kimekwisha kutokea
(kudhihirika)au bado hakijatokea lakini vile unaona ndivyo ulivyo.Maana yake
hapa kama unaona ukuu ndani yako tayari wewe ni mkuu ila kuna hatua ambayo
unatakiwa kuifanya tu ili kudhihirisha ile hali ilio ndani yako iwe katika
ulimwengu halisia.Moja kati ya hivyo kupata chanzo sahihi kitakacho kuwezesha
kuthibitisha hali yako ya ndani nje.Pia kama unaona madhaifu ndani yako maana
yake hivyo ndivyo ulivyo kwasababu hicho ndicho unachoona.Mtu alie na ukuu
ndani yake ana kazi ya kuuthibitisha maana matokeo ya ukuu hayawezi kuonekana
wala kufaidia kitu mpaka yamethibitika kwa watu wengine.Lakini mtu unaeona
mapungufu(mpumbavu) ndani yake wala hana kazi yeyote ya kukuthibitishia maana
utamuona tu jinsi anavyoishi,anavyo waza na hata usemi wake tu utamuelewa huyo
ni mtu wa namna gani.
UMESIKIA
NINI....TOKA KWA NANI?
Chanzo cha
taarifa mara nyingi ndio hua chanzo cha kuakisi na kukuaminisha kitu fulani
ambacho baada ya kukisikia, kuona au kusoma na kukiamini na kuiweka imani
katika matendo baada ya muda fulani wa mchakato matokeo huja vile vile kama
jinsi uliona au kuamini.
Inawezekana wewe
ulianza kuuona ukuu ndani yako....katika biashara, huduma, masomo, siasa au
uongozi, Sasa baada ya kuhisi kitu hicho ndani yako ni taarifa gani ulioipata
juu yako au juu ya ndoto yako? Je chanzo cha hiyo taarifa yako kilikua
sahihi? Ukijizoesha kusikia habari za
kushindwa basi unajijengea matokeo ya kushindwa kwasababu ubongo wako umekaa
tayari kupokea taarifa, kufikiri na kuifanya fikra kua imani na imani kua
katika matendo na kuleta matokeo halisi na kama kushindwa ndio imekua taarifa
yako basi jiandae kushindwa.
0 comments: