Milca kakete
Milca kakete hakumbuki vizuri ni umri gani alioanza nao
kuimba maana alikuwa mdogo sana pengine kati ya miaka 5. Aliongoza baadhi ya nyimbo katika kwaya iliyojulikana
miaka ya nyuma Tabora ambapo wimbo kama “yuko wapi aliyezaliwa” wengi wanajua
wimbo ila hawajui ni Milca aliyeimbisha wimbo ule...Utukufu kwa Mungu.
Mnamo mwaka 1999 na 2000 akiwa kiongozi wa sifa katika
Kanisa la Pentecoste Kurasini alipelekwa na Kanisa kuhudhuria semina ya
viongozi wa sifa nchini Kenya.Mwaka 2003 akiwa amehamia mjini Arusha,Mungu
akaongea naye kutoa album ya kuabudu inayokwenda kwa jina la “Yesu niko mbele
zako” na nyimbo nyingine ambazo zilipendwa
kama “Natamani kufanana nawe” “Nifinyange” na “Heri ni jina”
Kwa sasa Milca makazi yake ni Canada ambako bado anafanya
muziki wa injili kama kawaida na kupitia kituo cha VOA Sauti ya amerika
muziki wa injili kama kawaida na kupitia kituo cha VOA Sauti ya amerika
aliweza kuachia wimbo
wake mpya (NAKUNG’ANG’ANIA) ambao unatangaza album yake mpya ya (Video)
inayotarajiwa kutoka hivi punde siku za usoni.....unataka kujua mengi kuhusu
mwana Dada Milca Kakete endelea kufatilia Unclejimmytemu.blogspot.com kwa
habari kamili za Milca.Kwa hisani ya Uncle Jimmy nakupa nafasi ya kusikiliza
wimbo wake “Nakung’ang’ania” hapo chini
Picha zote kwa hisani ya Milca Kakete
0 comments: