Kushoto ni marehemu Dr.Askofu Moses Kulola akiwa na Askofu Mwaisabila
Siku
ya jana nili-post sauti ya Askofu Kakobe akisema kanisa la E.A.G.T baada ya
maziko ya Askofu Moses Kulola nchi nzima na mipaka yake litakua
likilitazama kanisa la E.A.G.T litafanya nini katika uchaguzi wa Askofu
atakayechukua nafasi ya Moses Kulola.Je, itakua sehemu ya kusaganasagana
na kukatana vipande?Alisema Askofu Kakobe.
Baada
ya kuzungumza hayo Askofu Kakobe katika kutoa salamu zake za mwisho,alisimama Askofu Mwaisabila na kusema mimi ndiye niliyekabidhiwa Ng'ata
na marehemu rafiki yangu Moses Kulola kama ulikua hujui. Nanuku-"Sasa
niwambie mimi badala yake yeye,mimi ndiye Baba yenu.Kama mlikua hamnijui
badala yake ametangulia rafiki yangu ameniachia kazi,kama ulikua na
kiburi nyweaga hapo hapo.Kama ulikua na kiburi ukawa una nidharau sasa
utanidharau namna gani".Mwisho wa kunukuu.
Maneno
haya aliyazungumza kwa msisitizo kama sehemu ya yeye kuonyesha umwamba
wake na kile alichoachiwa na marehemu Askofu Moses Kulola.Nisikuchoshe
sana msikilize hapo chini Askofu Mwaisabila.
0 comments: