Saturday, August 24, 2013

WATU WASIO JULIKANA WAMETUPA BOMO KANISA LA KKKT SEGEREA.

By Jimmy  |  10:05 PM No comments

 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ushirika wa Segerea limenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kutupa chupa iliyodhaniwa kuwa na mafuta ya taa au ya petroli na kulipuka ndani ya kanisa na kuunguza baadhi ya vitu vilivyowemo katika madhabahu ya kanisa pamoja na gari lililokuwa nje ya kanisa hilo majira ya saa 8 usiku usiku wa kuamkia leo.
 Akielezea tukio hilo mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Segerea Bwana Noaha Kipingu, amesema  limetokea majira ya saa 8 za usiku wa kuamkia leo ,wakati baadhi ya waumini wakiwa ndani ya kanisa katika maombezi ya yaliyoanza saa 4 usiku kwa ajili ya mkutano unaotarajiwa kufanyika jumapili ya agosti 25 mwaka huu.
Baadhi ya waumini walionusurika katika tukio hilo wamesema wamesikia mshindo mkubwa wa kitu kinachofanana na bomu katika madhabau ya kanisa hilo wakati wakiwa wamesimama mbele ua kanisa hilo na kisha moto ukaanza kuunguza madhabau hali iliyowafanya kukimbia na kisha kurudi ndani kwa ajili ya kuzima moto huo.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP