Askofu Thomas Laizer enzi za uhai wake
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini.Askofu Thomas Laizer amefariki duniaalasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.
Jana Februari 6, 2013 Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, alimtembelea na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini
Kati.
Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer
alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari
wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini hapo jana
saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari
wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalumu.
0 comments: