Kundi la kuchekesha la Orijino Komedi wanaofanya kipindi katika Television ya TBC 1 siku ya jana kupitia kipengele chao cha "Kukopi na kupest" wameibuka na wimbo wa Bibie Christina Shusho wa NIPE MACHO NIONE na VALU VALU wa muimbaji kutoka Uganda Jose Chameleone.
Jose Chameleone
Kipengele hiki cha orijino komedi cha kukopi na kupest uwa mahususi kwa waimbaji wanaopenda kunakirisha nyimbo za watu nakisha kuziimba wao.Kupitia kipindi chao jana wamekuja na wimbo wa Christina Shusho nakuonyesha jinsi gani Chameleone amekopi na kupest melody ya Bibie huyo nakubadilisha sehemu ndogo za wimbo huo.

Joti anaonekana kumkebei Masanja Mkandamizaji ambaye ameigiza kama Jose Chameleone katika kipengele hicho cha Kukopi na Kupest na kuonyesha jinsi gani Chameleone ameiba idea ya Christina Shusho kisha kutoka na record yake ya Valu Valu.Kwa tathimini za haraka albamu ya Christina Shusho ilitoka Mwaka jana 2011 mwishoni na wimbo wa Jose Chameleone umetoka mwaka huu mwezi wa Pili.
Christina Shusho.
Hii inanipa picha ya jicho la tofauti,kama Chameleone amechukua melody ya mwana Dada Christina Shusho je niwaimbaji wangapi wameibiwa melody zao pasipo kujua?.Nani hausike katika kuakikisha hakuna wizi kama huo unafanyika?.Je Christina Shusho anao uwezo wa kumshitaki muimbaji Jose Chameleone?.Hayo ni maswali niliyo baki nayo na bado sijapata majibu.
Sikiliza utani wa masanja na Joti katika komedi yao hapo jana.
Exclusive Uncle Jimmy.
Sikiliza utani wa masanja na Joti katika komedi yao hapo jana.
Exclusive Uncle Jimmy.
Hapo chini zipo Video Mbili ya kwanza ya kwake Christina Shusho inayofata ya Jose Chameleone .Zitizame vizuri nyimbo hizo kisha unipe maoni yako nani ameiba Melody ya mwenzake.
0 comments: