Tuesday, November 20, 2012

EXCLUSIVE INTERVIEW-MUUGIZAJI NA MFANYA BIASHARA DOTINATA ATAJA SABABU ZA YEYE KUOKOKA.KWA NINI ANATAKA KUFUNGUA KANISA?UTAJIRI MAGARI NA MAJUMBA NI JUHUDI ZAKE BINAFSI.

By Jimmy  |  8:00 AM 1 comment

Niliposikia Muugizaji Dotinata ambaye amejipatia umaarufu kupitia maigizo yake pamoja na kudhamini vitu vingi hasa upande wa mziki wa Bolingo au mziki wa Dansi na kuamua kumpa maisha yake Yesu Kristo,nilimtafuta ili tuweze kujua imekuwaje ameamua kumkabidhi Yesu maisha yake.

Kama Blogger nikafunga safari hadi Ubungo ambako ndiko anapoishi Msanii huyu,Mahojiano yangu na yeye yalikuwa marefu na hivi ndivyo ilivyo kuwa.

Uncle:Habari yako Dotinata 
Nikiwa kikazi zaidi na Mama Aliminata a.k.a Dotinata.

Dotinata:Nzuri ehee kumbe ni wewe naongea nawe kwenye simu daa kweli Yesu mzuri karibu Jimmy habari za siku.

Uncle:Nzuri Dada yangu leo nimekuja tuzungumze kidogo mana nasikia umempokea Kristo je ni kweli.

Dotinata:Ni kweli Jimmy.Nimeamua kuokoka ndugu kwakua kila anaeokoka ana historia,ukichunguza watu wote waliookoka wana historia.Kikubwa mimi nimeokoka kwakua Bwana Yesu ameniponya Mguu wangu niliohangaika nao kwa miaka minne bila kupona.Niliangaika na mguu wangu sehemu mbalimbali mpaka India lakini sikupona ndipo nikakutana na watumishi wa Mungu wakaniombea nikapona mguu.Hivyo sikuona sababu ya kuchelewa kumpokea Bwana Yesu kwa sababu ndiye aliye niponya.

Uncle:Sikiliza maneno yake juu ya kuamua kuokoka
 

Uncle:Baada ya kuamua kuokoka familia yako pamoja na ndugu zako wamelipokeaje swala lako mana najua ulikuwa umesilimishwa nakuwa muisilamu.
Mwendo ni uleule kikazi

Dotinata:Kwa upande wa ndugu zangu wamefurahi sana.Ujue Jimmy Mama yangu mzazi alimpokea Bwana Yesu miaka 20 iliyopita hivyo nilikuwa nikimkwaza Mama yangu pasipo kujua,mara kwa mara alikuwa akiniambia mwanagu naomba umpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako lakini nikawa nakata kilasiku.Lakini huwezi amini Jimmy ulifika muda nikasarenda mwenyewe bila kupenda nikaupokea wokovu na sasa nimeokoka naufuraia wokovu wangu.Kwa upande wa uisilamu nimeachana nao napia kwa upande wa vyombo vya Habari wamejua mwaka huu lakini ukweli nilisha mpokea kristo miaka mitatu nyuma ila kuamua kujitangaza imekuwa mwaka huu.
 Hi ni Sebule ya Mama Dotinata.

Uncle:Baada ya wewe kuamua kuokoka ndugu pamoja na marafiki zako walichukuliaje uwamuzi wako.  

Uncle:Kitu gani uwezi kukisahau huko nyuma kabla ujao okoka?Je ulisha wai kwenda kwa waganga wa kienyeji?

Dotinata:  
Uncle:Nimesikia unataka kufungua Kanisa kuna ukweli wowote katika hili.

Dotinata:Ilo naomba nikae kimya likitimia nitalitangaza kwa sababu ni jema nataka kweli ni mjenge Bwana nyumba ya Ibada naamini kwamba katika vitu vyote nilivyonavyo duniani hata kama nimejenga magorofa mangapi kama sito jenga nyumba ya Mungu bado nitakuwa sijaridhika ndani ya moyo wangu nanitakuwa sijamtendea Mungu haki.

Uncle:Nini siri ya mafanikio yako?

Dotinata:Jimmy siri ya mafaniko yangu nikufanya kazi kama punda bila kujali unapata shilingi ngapi lakini kikubwa namshukuru mwenyezi Mungu sana namshukuru Yesu wangu sana toka nimebadilika kumpokea Bwana Yesu nimekuwa nikishika pesa zangu nikiziona.Nimekuwa nikifanya mambo ya maendeleo zaidi natumaini nimeweza kufanya vitu vingi kwa muda mfupi naamini pesa nilizokuwa napoteza kwa waganga kwa marafiki kwenye pombe kwenye miziki ya Duniani sasa nitazitumia vizuri katika kuendeleza miradi yangu mikubwa.

Uncle:Una vitu gani Dotinata unamiliki kwa sasa.

Dotinata:Mimi ni mjasiliamali nina miliki vitu vingi,namiliki magari makenta,fuso,majumba ambayo Mungu ameweza kunibariki ninaweza kuzipangisha kwa watu.Nina gari ninazo fanya kama tuwazi ambazo ni HUMMER,RANGE,VOGI na MERCEDES BENZ ambazo nazitumia kwenye mambo ya maharusi namshukuru Mungu kiukweli.
 
 Hapa ni gorofani anakoishi Dotinata

 Uncle:Labda ni nyumba ngapi unamiliki?

Dotinata:Nisiri yangu.........

Uncle:Nimesikia kwa sasa una Record albam ya Gosple nikweli.

Dotinata:Nikweli Jimmy kwa sasa nimesha Record nyimbo 4 na ya kwanza nimesha iyachilia katika vituo vya Radio unaojulikana kama "BARAKA ZA BWANA" hata hivyo niko mbioni kufanya Video za nyimbo hizo zote nne nikimaliza nitarudi tena Studio kumalizia nyimbo nne kisha niweke albam mtaani.

Kulia ni Mama Mchungaji anaye mlea Dotinata kwa sasa.
Uncle:Watu gani unawapa shukrani mpaka hapa walipo kufikisha.


Dotinata:Wako watu wengi wakuwashukuru wa kwanza ni Mama yangu mzazi ambaye alikuwa akifunga na kuomba kila siku ili mimi niokoke,Pili namshukuru Mungu kwa neema ya Wokovu aliyo nipatia mimi.Mana Biblia inasema Jimmy tunaokolewa kwa neema hivyo nina kila sababu ya kumshukuru Mungu.Tatu nawashukuru watumishi wa Mungu walioniombea mguu wangu ukapona,Mungu awape haja ya mioyo yao na waishi milele kwa utukufu wa Mungu.Nne nakushukuru wewe kuja kwangu leo nimefurai kukuona naamini yapo mengi nitajifunza kwako na utanisaidia katika kazi ya mziki wa Injili.Tano wasoma  wote wa Blog yako.Barikiwa.

Uncle:Asante sana Dada yangu kwa time yako nzuri yakukubali watanzania na watu wote Duniani kutambua wewe sasa ni mteule wa Bwana rasmi na pia kuniruhusu mimi kufanya mahojiano haya na wewe.Naamini kukiwa na jambo hutosita kunifahamisha.

Dotina:Amina Jimmy hivi siku hizi uigizi tena.

Uncle:Siwezi kuacha mpaka Yesu anarudi Dada yangu,mambo ya mekuwa mengi ila mdogo mdogo siku moja wataelewa tu.Siku njema.
PICHA SITA ZA POZI LA MAMAA DOTINATA NAKATI YA UBUNGO.









Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

1 comment:

  1. Thanx Jimmy for sharing this, watu wengi walizungumza yao bila kuwa na taarifa kamili

    ReplyDelete

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP