Tuesday, October 9, 2012

WAZAZI WA MWANAMUZIKI ALIETOKA FAMILIA YA KUMCHA MUNGU (LINAH SANGA) WAZAZI BADO WAMLILIA KUBADILI MAVAZI AVAHAYO.

By Jimmy  |  12:13 AM No comments

Muimbaji Linah Sanga,alietoka katka familia ya kumcha Mungu mpaka kuimba Bongo freva amedai kuwa huwa anapoenda nyumbani kwa wazazi wake huwa anavaa nguo ndefu tena za kilokole ili asije kuwaudhi wazazi wake ambao wamemkuza katika maisha hayo.

Msanii huyo anapenda kuishi kizungu baada ya kuigia kwenye muziki wa Bongo freva, ingawa anadai kuwa hawezi kusahau maisha ya dini aliyokuwa anaishi awali ambayo yalikuwa yanamfanya avae nguo za heshima tofauti na sasa.
Baba mzazi wa Linah pamoja na Mama mzazi.

Linah akizungumza na Radio moja hapa mjini alidai kuwa tangu alipoachana na wazazi wake maisha yake yamekuwa tofauti kwani muziki kwa upande fulani umebandilisha maisha yake, kuanzia kwenye mavazi tabia na hata lifestyle.

“Napozungumza tabia haimanishi nimekuwa muhuni hapana, bali awali nilikuwa sijuani na watu maarufu lakini sasa nimekuwa nao karibu na kuna baadhi ya vitabia nimekuwa navyo lakini si kwa ubaya,” alidai na kuongeza 
 
"Na  ninapoenda  kuwaona  wazazi  hunilazimu  nivae  kilokole  maana  sipendi  kuwakwaza"

Msanii huyo aliongeza kuwa wazazi wake wamekuwa wakimsihi sana kuvaa nguo zile zile za zamani lakini haoni kama zina nafasi kwa sasa kutokana na career aliyoichagua. 

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP