Monday, October 29, 2012

HIKI NDICHO ALICHOSEMA ROSE MUHANDO SIKU YA JANA MJENGONI KUHUSIANA NA ALBAM YAKE MPYA "KUNG'UTA YESU"

By Jimmy  |  10:57 AM No comments

Kama ulifatilia show ya jana nilipokuwa na Rose Muhando ni mengi aliyo eleza kwa habari ya mziki wake.Kubwa alilonifurahisha ni kuhusiana na albam yake mpya aliyo fanya Afrika Kusini na Tanzania.Malikia wa mziki wa Injili alisema kuwa kwa sasa albam yake imesha kamalika ikiwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya SONY.
Malikia wa Mziki wa Injili Rose Muhand.

Albam hii yenye jina la 'KUNG'UTA YESU' yenye nyimbo 8 zikiwa Tatu amefanya hapa Tanzania na Tano akiwa amefanya Afrika Kusini akiwa ameshirikiana na waimbaji maarufu kama {Solomoni Keke na William Sejake}Kupitia albamu hii Rose Muhando alisema kuwa watu wakae mkao mzuri kupata raza mbili tofauti kwa muimbaji Solomoni Keke aliye imba Kiswahili pamoja na Kizuru.

 Rose anasema kuwa yapo mambo mengi amejifunza kupitia wanamuziki wa Afrika Kusini kutokana na wao kupiga hatua kubwa katika uimbaji.Jambo kubwa alilo jifunza ni wao kuimba kupitia mtindo wa Live Band ambao yeye ameuchukulia kama changamoto katika maisha yake.
  Mwana wa Aron akiwa na Bibie Rose Muhando siku ya jana

Kwa sasa Rose Muhando yuko katika kujipanga kufanya Video za nyimbo mbili nchini Afrika Kusini nchini ya Kampuni ya Sony.Ukiachana na kazi ya mziki anayoifanya Rose yuko mbioni kufanya Filamu ya maisha yake aliyopitia toka alipo anza mziki mpaka apo alipofika.Filamu hii itasimamiwa na Sony wakishirikiana na baadhi ya waigizaji kutoka hapa Tazania.Nishauku yake kubwa kufanya Filamu hiyo kwakua ni moja ya Ndoto zake siku moja afanye Filamu itakayo badilisha maisha ya mtu mmoja aliye kata tama kutokana na umasikini anao pitia.

Mwanzoni mwa mwezi wa 12 mwaka huu Rose Muhando ataachia nyimbo moja kutoka katika albam yake mpya itakayo ambatana na Video ya wimbo huo.

Albam hii ina nyimbo Nane 1)Majira ya Jioni 2)Kwa Yesu kuna mambo 3)Yesu Jiwe 4)Yerusalem 5)Hallelujah Hosana 6)Sondezigue 7)Shine na Papa 8)Wololo

Nyimbo Sondezigue amefanya na Solomoni Keke,Hallelujah Hosana amefanya na William Sejake.Wimbo Wololo una mana-Tusafishe Baba,Sondezigue-Nivute uweponi mwako
 Listar Kulanga akiwa na Rose Muhando
Baada ya maojiano kuisha RoseMuhando akitupa kionjo cha baadhi ya nyimbo zake.

Kupitia Blog yako utapata kusikia Record yake mpya soon atakapo iyachia

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP