Yapo matoleo ya waimbaji wa mziki wa Injili ambayo yameingia sokoni yana mwezi mmoja au miwili lakini ujio wao aupo vizuri kama ujio wao wa mara ya kwanza.Uwa najiuliza maswali nasipati jibu,kwa nini albamu ya kwanza ya muimbaji wa mziki wa injili uwa nzuri sana lakini inapofata ya pili nakuendelea uwa za kawaida.
Leo niliamua kupita maduka mawili matatu kuuliza nani anafanya vizuri sokoni kwa habari ya mauzo na albamu gani mpya imeingia kwa sasa.Zipo albamu ambazo zina muda madukani lakini kutokana na Radio station kupiga nyimbo zake mara kwa mara imesababisha albamu ya muimbaji huyo kutafutwa kwa wingi na mauzo yake kuwa mazuri.
Hii ni albamu mpya naya pili ya Martha Mwaipaja iliyoingia sokoni mwezi mmoja tu.Inafanya vizuri sokoni kutokana nakupata air time nzuri kwenye radio station za Bongo na mikoani.Ina semekana ni muimbaji peke anaeuza vizuri kwa sasa sokoni.
Unclejiimmy inakupongeza Martha kwa ujio wako wa pili uliokuja vizuri radio na sokoni.
Hii ni albamu yake ya Tatu ambayo ametoa DVD pamoja na Audio CD nae nimoja kati ya waimbaji wanaofanya vizuri sokoni na radio.Kwa sasa radio anatamba na wimbo wa Moyo wangu na Yesu jina zuri.
Huyu ni Mchungaji na muimbaji ambaye wiki nne nyuma ametoa albamu yake sokoni pamoja nakuleta wimbo mmoja radio {Usinipite} unaobeba jina la albamu kama inavyo onekana.
Atosha Kissava.
Atosha Kissava nae ni muimbaji alietoa Video cd ikiwa na wiki mbili,kwa sasa inapatika madukani kote.
Hii ni albamu ya muimbaji wa Bondeni kwa Madiba Solly Mahlangu ambaye albamu hii inaweza ikawa na mwaka mmoja sasa lakini kupitia wimbo wake wa Together as one uliopo katika albamu hii umeleta gumzo kupitia vituo vya radio za Dar kutokana na kupendwa na wasikilizaji ivyo kufanya kwa siku moja kupigwa zaidi ya mara 10 kwa siku nakupelekea kufanya vizuri sokoni.
Moja kati ya albamu zangu kipenzi ni hii Spirit of Praise.Ni mchanganyiko wa waimbaji wa afrika kusini akiwemo Benjamin Dube,Solly Mahlangu,Zaza,Tshepiso,Andile b,na Marl.Ni bonge moja la albamu iliyo sheheni Star wa afrika kusini na nyimbo za ukweli.
Albamu hii ina mwaka mmoja toka iingie sokoni lakini kupitia wimbo wa Benjamin Dube wa Kiti wena unaopendwa na wasikilizaji wa Praise power fm kwa sasa inafanya vizuri sokoni na vituo vya radio station za hapa Dar.
Dan ni muimbaji aliyeamua kutumia aina ya mziki wa Gita katika kuzirudia Tenzi za rohoni.Albamu hii ina miezi 7 tangu iingie sokoni na kwa sasa inapatikana madukani kote.
Hizi ni moja kati ya albamu za wana muziki wa injili zilizo toka miaka miwili au mwaka mmoja nanusu lakini kwa kiasi flani bado zinatamba masikioni mwa watu.
0 comments: