EXCLUSIVE MCHUNGAJI KIONGOZI
KARIBU MLIMA WA MOTO.
Eneo la packing kwa waumini wa Mlima wa Moto.
Mchungaji kiongozi Dr Getrude Pangalile Rwakatare wa Mlima wa moto Mikocheni "B" Ass of God.
Ibada imeanza rasmi
Waumini wa Mlima wa Moto wakisikiliza mafundisho ya neno la Mungu kwa makini sana.
Ibada ikizidi kuendelea na waumini wakiwa watulivu sana
Wakati ulifika wa kuombea mahitaji kama picha inavyoonyesha hapa
Mchunga kiongozi akiwa amebeba mahitaji kwaajili ya maombi
Kitendo tu cha kuanza maombi gafla binti huyu alianguka chini na wahudumu walimuwahi na kumuhudumia
Hawa nao walipatwa na nguvu ya Mungu kisha kuanguka chini
Jopo la wachungaji wa Mlima wa MOTO WAKIOMBEA MAHITAJI
Mzee wa kanisa Mzee Mathemba.
Baada
ya maombi zoezi la kuinadi albamu ya Happy Kwaya ilianza na kila mtu
alipenda kushiriki baraka za bwana na hapa katika picha tunamwona Mzee
Mathemba ndiye aliyepewa dhamana ya kulisimamia zoezi hili
Baada
ya zoezi la kuinadi albamu ya Happy kwaya kumalizika na hapa ni Obama
mtoto wa mchungaji akishiriki baraka kwa kutoa Tsh 2milioni.
Mc wa zoezi hilo Victor Aron
Yote kwa yote ibada ilihitimishwa kwa kugawiwa damu ya yesu kama picha inavyoonekana
Katika
kujifunza na kuona ni jinsi gani damu ya yesu ina nguvu kwa maisha ya
mwanadau waweza kujifunza zaidi katika maandiko Yohana 6:57-58 pia
Zaburi 105:3-37,Isaya 11:1-2 lakini kama hiyo haitoshi waweza jifunza
katika 2Wafalme 4:38-40-41 na masomo mengine kama Luka 30:20-24,Ufunuo
12:11,Luka 22:19-20 na Isaya 40:23-25 na mengine mengi kama hayo.Hakika
tamani sana kunywa damu ya yesu itakuponya kila kitu katika maisha
yako.MUNGU AKUBARIKI
Souce Blog Erick
Wacheni mahubiri ya kimwili. Mungu ni Roho na wote watakaomwabudu inawabidi wamwabudu katika Roho. Kasema Yesu. Hii Ibada ya kunywa mizabibu na divai ni ibada ya mwili na haina manufaa katika Roho. Mwaongoza wanadamu ka njia ya mwili na vituko na mahubiri ya kimwili huku mkijifanya wachungaji. Kwa nini msihubiri wokovu uletao toba especially nyakati hizi za mwisho wakati Yesu anaandaa kunyakua kanisa. Nyinyi mwahubiri kufanikiwa, kuoa na kuolewa, kujenga, na kadhalika. Hizo hazina umuhimu nyakati hizi za mwisho. Yesu anataka mtayarishe kanisa kwa unyakuzi.
ReplyDelete