Tuesday, July 10, 2012

MWAKA MMOJA WA UNCLE JIMMY

By Jimmy  |  6:00 PM No comments

Ipo sababu ya kumshukuru Mungu kwa hatua niliyochukua mpaka hapa nilipofikia mwanzo nilipata upinzani mkubwa lakini sikuangalia vikwazo vya watu wanasema nini nikafunga mkanda nikasonga mbele.Siku ya Tarehe 1/7/2011 Blog yangu iliweza kuzaliwa katika Hotel ya Atriums kwa Shigongo.

Ilikuwa kama utani wakati naanza kuifremu jinsi itakavyokuwa lakini ashukuriwe Mungu now imefikia Mwaka mmoja,Ni ukweli usiopingika kazi ya Blog inahitaji kujituma na kuipenda kama Baba apendavyo watoto wake/wawili wapendanao.

Wapo watu ambao naomba niwashukuru katika kuhusika na hatua ya mwanzo katika kuitengeneza Blog.Wakati naanza kutafuta mtu wa kuitengeneza Blog yangu alikuwa Kijana Victor Sostenes Langula.

Victor Langula alihusika Mwanzo wa Blog yangu kudesgn mpaka kuakikisha inaonekana muonekano mzuri kwa mwanzo.Victor alipata tabu sana baada ya kunikabidhi Blog yangu.Maana kila ilipokuwa inasumbua sikuacha kumpigia simu,nae hakuacha kunielekeza nini chakufanya.Kwa sasa Victor amehamia Zanzibar Unguja akiwa kikazi zaidi.
Jembe Victor

Safari ikaendelea mdogo mdogo nikijifunza jinsi yaku-post Story na Techinical za Blog,Mara Victor Langula akahamia Zanzibar,ilikuwa kazi kubwa kwangu mana nilijiuliza maswali kitu kikinishinda nitafanyaje?Lakini ashukuriwe Mungu maana alinipa rafiki mwingine aliyenitia moyo na kunifundisha mambo mengi sana katika Blog.

Kijana huyu ambe sasa yupo mkoani Arusha akitamba na Blog yake ya OHAYODA.BLOGSPOT.COM si mwingine ni Amani Paul.Yeye aliweza kuongeza muonekano mzuri wa Blog.Akaongeza Picha na kubadili rangi ya nyuma ya Blog.Hiyo haitoshi siku ya uzinduzi wa Blog yangu kwa mara ya kwanza yeye alisimamia zoezi zima la kuhakikisha kila alie fika katika kushuhudia uzinduzi huo anaona kila kitu kwa ustadi mzuri.
Techinical Amani Paul.
Hii ni Picha ya muundo wa Blog yangu wakati ikiongezwa mnogesho na Amani Paul.
Hivi ndivyo ilivyo kuwa katika Ofisi ya Amani Paul enzi hizo The Bridge.

Lakini bado wapo watu wengi ambao wamenisaidia mambo mengi katika Blog yangu.Sam Sasali amekuwa mtu wangu wa karibu sana kunisaidia mawazo,ushauri,na hata pale ninapokosea haachi kunikosoa.
Sam Sasali.

Noel Tenga moja kati ya wadau wakubwa wa Blog yangu amekuwa akinisaidia mambo mengi sana kama muhariri wangu.
Kaka Noel Tenga.

Sitoweza kumsahau Victor Mboya ambaye amekuwa akinisaidia vitu vya kiufundi hasa pale katika kunogesha Blog kwa wewe msomaji.
Mwana Harakati Victor Mboya.

Lakini ukiacha Historia ya Blog hii liko jambo ambalo nataka kushirikiana na wewe my lovely Friend ambae umekuwa ukipita na kupata Story mbalimbali na burudani hapahapa katika www.unclejimmytemu.blogspot.com.

Tarehe 20/7/2012 nafanya Event katika Hotel ya Tamal nikimshukuru Mungu kwa jambo jema la Madhabau ya Blog yangu kutimiza Mwaka mmoja.Hivyo nakuomba wewe rafiki yangu tushirikiane kwa pamoja katika shughuli hii,Kikubwa nahitaji mchango wako ilikuweza kupata vifaa vitakavyoweza kuniwezesha kupata Habari kwa urahisi na hata kufikia watu wengi katika kufikisha Habari kwa jamii.

Event hii ni bure hakuna kiingilio chochote ni wewe na miguu yako,Dar-es-Salaam Band ndio watahusika kuhakikisha wewe unacheza nakufurahi siku hiyo,Flora Mbasha na Mumewe watahusika katika kupamba siku hiyo.Karibu sana rafiki na Mungu wa mbinguni akubariki.
Uncle Jimmy

Waweza tuma mchango wowote ku-support Blog hii kwa Tigo Pesa kwa No O713-763939/0713-494110 atuna kadilio la kiasi cha fedha kadili moyo wako utavyo guswa karibu .



Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP