Saturday, July 28, 2012

MANENO 8 YA PASTOR MYAMBA KATIKA RISE AND SHINE.

By Jimmy  |  6:25 PM No comments

Hapa alikuwa akinipa kibwagizo cha moja ya maneno yaliyoko katika filamu yake.

Kupitia kipindi kikali cha Rise and Shine ninachokiendesha mimi na swahiba wangu Erick Martin .Haya ndiyo maswali aliyojibu Super Star Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba.

1}Ziko tetesi wanazosema wewe ni Freemason?
 Myamba-Uncle hayo siwezi kuyasema ila waje ofisini kwangu niwape neno lenye pumzi ya uzima litakalo badili fikra zao potofu.

2}Filamu  zako unadhani zinaweza kuwaleta watu kwa kristo?
Kaka 80% Filamu zangu zina uwezo mkubwa sana kubadili maisha ya kila mtu  asiyeokoka.Mimi naamini kupitia neno la MUNGU na neno lina uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu kupitia filamu.

3}Unafikiria kupitia stahili yako ya {Pastor} inaweza kudumu katika sanaa  au unampango gani uko mbele kubadili aina ya uigizaji ili uweze kufikisha ujumbe tofauti kwa hadhira inayokutazama?
Aaa kiukweli sina wazo ilo ila ninacho fanya nataka kuwa mbunifu katika kila Filamu zangu ninazofanya na Kampuni yangu ili nimpatie mtazamaji kitu kilicho na ubora.

4}Unawasaidiaje wasanii wachanga?
Kaka zangu nilishajaribu kuwasaidia  wasanii wadogo lakini nilipata shida sana kwenye Shooting.Mtu anakuja anakuambia anakipaji akishafika kwenye setting anaanza kutetemeka badala ya kuanza kuigiza.
-Nilichofanya kwa sasa nimefungua chuo changu cha sanaa ambacho msanii akifika anafundishwa miezi 3 halafu miezi 3 shooting.Hii kwangu ni njia rahisi ya kuwasaidia hawa wenye kipaji.

5}Unadhani miaka 5 mbele Emmanuel Myamba atakuwa wapi?
  Kwa sasa Sanaa imepiga hatua.Na malengo yangu niliyoyaweka naamini yatatimia kama tutakuwa wazima na nina malengo ya kufika mbali sana na kufananishwa na waigizaji wakubwa wa hapa duniani.

6}Wasanii wengi wanaokoka lakini wanashindwa kudumu kwenye wokovu wewe unadhani tatizo liko wapi?
Ni ukweli usiopingika Uncle wengi huja kwakubeep tu,Na kingine hawana wachungaji wakuwasimamia hivyo hilo ni tatizo kubwa sana.

7}Kuna usiano upi kati ya Filam yako ya Gods Kingdom na Devils Kingdom ya Marehemu Stevin Kanumba?
Kabla marehemu Kanumba hujafariki nilisha kutana nae nikamuomba nimjibu kupitia Filamu yangu ya God's Kingdom.Sababu ya kumuomba ilikuwa filamu yake imeonyesha shetani anavyojinyanyua wakati hana uwezo mbele za Mungu,kwa hiyo hilo ndilo kubwa nililolenga kuakikisha Mungu anajitwalia utukufu wake.

8}Watu gani unawashukuru mpaka hapa walipokufikisha?
Mtu wa kwanza ni marehemu Stevin Kanumba,Produz Mtitu,Dada yangu wa kuzaliwa nae na Mashabiki wangu bila kumsahau Apostel Onesimo Ndegi.

PICHA 6 TOFAUTI AKIWA STUDIO ZA 99:2 PRAISE POWER RADIO KWENYE SHOW YA RISE AND SHINE.
 Hii ni tabu aliyoipata baada ya kutoa namba ya Simu hewani 
 Hapa sijui nilikuwa nasoma nini
 Emmanuel Myamba

Gari anayotumia kwa sasa kama usafiri wake binafsi.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP