Thursday, August 21, 2014

VIDEO:MLEMAVU WA NGOZI YA ALBINO "BI MARIAM" ALIYEKATWA MIKONO YAKE KWA IMANI ZA KISHIRIKINA.

By Jimmy  |  6:29 PM No comments

Majira ya saa 7 usiku Mariam alisikia Kishindo cha Mlango "Puuu" akastuka kutoka usingizi. Akapaza Sauti Kumuita mdogo wake mwenye jina la Reuben kama ndiye aliyefungua mlango, Reuben akasema lla hasha si yeye aliyefungua mkono.alipokuwa katika hali ya kujiuliza nini kinaendelea akaona ni vema kwenda sebuleni. Kwa maisha ya kijijini aliamua kuwasha kibatari ili kuweza kupata mwanga. Alipokuwa anataka kutoka nje moyo wake ulisita sana akaamua kuchungulia dirishani kwanza. Aliponyemelea dirisha ghafla nyuma yake akahisi kivuli cha mtu alipogeuka ana kwa ana akakutana na uso wa jirani yao wa siku nyingi Mr. George akiwa ameambatana na watu wengine chumbani kwake. Katika hali ya taharuki akaanza kupiga kelele na muda huo huo Mr. George akazima mwanga wa kibatari kisha akamkamata Bi Mariam Mkono na kuanza
kuukata na Panga lanye makali. Mr. "George" akafanikiwa kuukata Mkono wake kisha kuwapatia watu waliioambatana nao. Baada ya kumaliza akamwita Bi Mariam kwa jina kuwa ageuke amkate mkono wa pili.
na purukushani Mr. "George" hakufanikiwa kuukata wote na kisha waliamua kuondoka pasipo umalizia mkono huo ulibaki ukiwa unaning"inia tu. Muda wote wazazi wake walibaki kupiga kelele tu kwa sababu milango yao ilikuwa imefungwa kwa nje. Kelele za Mariam pamoja na Wazazi ziliamsha majirani waliamua kwenda nyumbani kwa akina Mariam.USIKOSE KUTAZAMA KISA HIKI CHA KUSIKITISHA J/PILI 27/8/2014 CLOUDS TV....Kuanzia saa 12:oo hadi saa 1:oo usiku kwenye kipindi cha CHOMOZA YA CLOUDS TV

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP