Thursday, August 28, 2014

MAKUTANO YA TAI na JAMES KALEKWA.

By Jimmy  |  7:36 AM No comments

 Ongoza kimkakati
 
Mfano wa lengo ambalo ni SMART: Kuihubiri injili kwa watu 1000 nchini Tanzania katika wilaya 4 kwa mwaka mmoja.
Je, lengo hilo ni hususani (Specific)? Ndiyo kwasababu limetaja idadi ya watu,idadi ya wilaya na nchi.
Je, lengo hilo Linapimika
(Measurable)? Ndiyo kwasababu ya idadi, eneo la kijiografia (mahali) yaani mwisho wa siku unaweza kukaa chini na kuangalia kama wilaya 4 zimefikiwa na kwa kiasi gani, vilevile kuona kama watu 100 wamefikiwa.

Je, lengo hilo linafikika (Attainable)? Ndiyo, kwa Jiografia ya Tanzania inawezekana kuzifikia wilaya hizo kwa muda huo. Pia unaweza kupata muda wa kujiandaa, kifedha, kimaombi, ujumbe kwani mwalimu mzuri ni mwanafunzi wa kudumu, kwahiyo lazima ujifunze ili ukafundishe.
Je,lengo hilo linauhalisia  (Realistic)? Ndiyo, kwasababu muda unaruhusu kufanya mambo mengine kama maandalizi ya uwanja/ukumbi wa mikutano, mahali pa kufikia, watu wa kushirikiana nao (si unajua huwezi kushirikiana na watu wote na kwa upande mwingine huwezi kushirikiana na kila mtu?) n.k yaani kwa lugha ya kiingereza wanaita "logistics", pia unaweza kuwa na muda wa kutimiza wajibu wako mwingine kama baba/mama (mzazi), kama mme/mke, kama mtoto na vitu vya msingi kama hivyo lakini pia kuna jambo la muhimu ambalo watu wengi hulipuuzia,lakini ni la muhimu sana...MAPUMZIKO! Mungu baada ya kutenda kazi siku sita alipumzika! Umuhimu wa kupumzika ni kwamba unaporudi tena kwenye utekelezaji, unakuja na nguvu mpya "fresh". Mungu akusaidie kuyaelewa haya na kuyatendea kazi na maisha yako hayatakuwa kama yalivyo, na hayo ndiyo maombi yangu kwa Mungu kwaajili yako msomaji wangu.

 Mifano hai ya watu waliotutangulia.

·                     Bwana Yesu
         Bwana wetu Yesu Kristo aliacha enzi na utukufu wake huko mbinguni na kuja duniani kufa badala yetu ili atukomboe kutoka katika laana ya dhambi.Ukitazama katika upana wa yale aliyoyafanya Yesu akiwa duniani utaona kuwa jambo jingine alikuja kuweka msingi wa maisha (kielelezo) ambayo watu wote waliomwamini wanapaswa kuyaishi kwa lugha ya kiiengereza tungeweza kusema Yesu ni role model wa maisha ya imani hii tuliyonayo!
Bwana Yesu hakuishi maisha ya kubahatisha, bali alikuwa na malengo; hebu jiulize nini kilimfanya aanze huduma akiwa na umri aliokuwa nao (miaka 30) na wala si vinginevyo? Kwanini alichagua wanafunzi kumi na mbili na si ishirini, watano au arobaini? Kwanini alikufa wakati huo na si wakati mwingine? (Wakati mwingine Wayahudi walikuja kumkamata Yesu ili wakamshitaki kisha wamuue lakini mwenyewe alisema wakati wake haujafika, akapita katikati yao na kuwaacha)
Ukisoma kwa umakini maombi ya Bwana Yesu kwaajili ya kanisa lake katika Yohana 17:1-26, utaona mambo ya uhakika juu ya vitu alivyokuwa akivifanya mstari 4, "Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye." Bwana Yesu anaupata wapi ujasiri wa kujua kazi amemaliza wakati alijua wazi kabisa kuwa kuna watu wengi tu walikuwa hawajaokoka bado? alikuwa hajafika sehemu zingine mbali na Mashariki ya kati (Afrika alikuwa bado hajafika,Asia,Ulaya n.k), sasa kwa hali ya kawaida Yesu alikuwa bado hajamaliza kazi lakini malengo yote yanapaswa kuwa na ukomo wa muda. Hapo baadaye katika sura hii kwa kadri ya neema ya Kristo nitakufundisha mambo yakuzingatia unapoweka malengo na sifa za malengo mazuri. Nakushauri uzisome kwa upya tena injili nne kwa lengo la kutazama maisha ya Bwana Yesu na malengo.
·                     Mtume Paulo
 

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

0 comments:

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP