Thursday, June 5, 2014

MAKUTANO YA TAI NA JAMES KALEKWA.

By Jimmy  |  7:10 AM 1 comment

Jifunze kuutumia msimu wa maamuzi unufaike!




i.                    Maisha baada ya kifo

 Biblia kwa namna nyingi sana inatuthibitishia ya kwamba kuna maisha baada ya maisha haya ya sasa na maisha yajayo baada ya haya ni maisha yaliyo na umilele- yaani yasiyo na mwisho! Lakini si watu wote tutakuwa na maisha sawasawa katika ulimwengu wa maisha baada ya kifo, kutakuwa na makundi mawili makubwa: mkono wa kuume na mkono wa kushoto; kondoo na mbuzi; wema na waovu;
paradiso pamoja na Mungu au ziwa la moto pamoja na shetani na malaika zake. Maisha ya milele yatakuwa na pande mbili tu na habari njema ni kwamba pande zote zitakuwa ni za milele.
Katika muhula huu wa maisha hakuna muda wa kufanya maamuzi na tena si muhula sahihi kufanya maamuzi. Pia ni muhimu kutambua ya kwamba muhula huu ni muhula wa kuvuna kutoka kwenye muhula wa pili wa maisha, kuwajibika juu ya ukataji wa maneno ulioufanya wakati wote ulipokuwa ndani ya bonde.
Waebrania 9:27
“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.”
Mwandishi waraka kwa Waebrania analeta picha ya kisheria na kimahakama ya kwamba baada tu ya kufa ni hukumu. Kwa uelewa wa shughuli za kimahakama lazima ujue ya kwamba hukumu haitolewi kutokana na matakwa, maoni au fikra za upande mmoja (jaji, utetezi na mashitaka) bali maamuzi ya mahakama yaani hukumu hutolewa kwa kuakisi ushahidi uliotolewa mahakamani. Kwa namna nyepesi ya kueleweka ni kwamba jaji hutumia jumla ya ushahidi kama ukweli (facts) na malighafi ya kufanya maamuzi ya kimahakama. Kwahiyo, jaji/hakimu hatoi maamuzi yake hewani bali kwenye maisha ya mshitakiwa husika. Kwa mfano mwepesi ni kwamba hakuna mahakama duniani inaweza kunihukumu kwa kesi ya uhaini hata kama utolewe ushahidi uliojaa vitabu vikubwa (volumes of books). Hakuna mahakama inaweza kumuhukumu kifo ndugu Joshua (nimetumia jina kutolea mfano) hata kama kesi itakuwa na mashahidi milioni moja. Kwanini? Kwasababu hakuna alama hiyo kwenye maisha yangu; hakuna mtiririko huo kwenye maisha ya ndugu Joshua. Si kwamba mahakama haina uwezo na wala si kwamba hakimu/jaji ana mamlaka kidogo, bali ni kwasababu maisha yetu hayastahili hukumu hiyo. Kitu ninachotaka uone ni kwamba kimsingi anayeamua mwenendo wa kesi au aina ya hukumu ni muhusika (mshitakiwa) na si mtu mwingine yeyote.
Hebu nikuonyeshe mfano wenye maelezo mengi zaidi kutoka kwenye kinywa cha ahukumuye kwa haki, Yesu Krsito mwenyewe.
Luka 16: 25-26
“Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo hivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.”
Kuielewa vizuri hii habari unaweza kuirejea kutoka kwenye mstari wa 19 mpaka wa 31. Utaona ya kwamba mistari niliyoiweka hapo juu ni matokeo baada ya maisha ya Lazaro na tajiri wakiwa duniani. Kosa la yule ndugu halikuwa utajiri bali ilikuwa ni nia yake atumiapo utajiri ule, “…aliyevaa  nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa…”. Siku zote za maisha alikuwa na nia ya kufanya anasa- alivaa na kula kwa anasa! Lakini Lazaro hakuwa na nia ya anasa, kula na kuvaa kwake kulikuwa ni kukidhi mahitaji muhimu… Nia zao kuelekea chakula na mavazi zilikuwa ni tofauti, umeona, eeh?
Baada ya kufa ndiyo wanakutana katika maisha ya milele lakini wakiwa kwenye pande mbili tofauti. Kitu gani kiliamua utofauti huo? Hakuna sehemu Biblia inatuambia kwamba baada ya kufa walifika mahala pa njia panda na kupewa nafasi za kuchagua wapi watumie maisha yao ya milele, hakuna! Maisha yao ya baada ya kifo yaliamuliwa na mfumo wa maisha yao kabla ya kifo – kuwa kifuani mwa Ibrahimu au kwenye mateso ni uamuzi wao wenyewe (tajiri na Lazaro) na uamuzi huo hufanyika kwenye maisha kabla ya kifo. Kitu ninachotaka ujifunze hapa ni kwamba maisha ya baada ya kifo si sehemu ya kufanya maamuzi wala kujitafutia fursa ya kufanya hivyo! Baada ya kifo ni hukumu na hukumu hiyo inatokana na vile maisha ya kabla ya kifo yalikuwa.

Author: Jimmy

Hello, I am Author, decode to know more: In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In commodo magna nisl, ac porta turpis blandit quis. Lorem ipsum dolor sit amet.

1 comment:

  1. Casino no deposit bonuses, casino games to play free online
    The casino no deposit bonus is one you need to know about before you are playing. It is a air jordan 18 retro men red sale really popular 스포츠토토 사기 벳피스트 way air jordan 18 retro men blue to my site of playing online 슬롯 머신 casinos and is not best air jordan 18 retro men blue only a great

    ReplyDelete

E-mail Newsletter

Sign up now to receive breaking news and to hear what's new with us.

Recent Articles

© 2014 Uncle Jimmy | Distributed By My Blogger Themes | Created By BloggerTheme9
TOP