Josphe Nyuki ambaye alitamba na nyimbo zake kama Umwema Mungu,Bwana Yesu ni tgemeo langu,Mambo kwa Yesu, kwa sasa yupo na makazi mapya nchini Kenya...May 18,2012 niliandika story ya maisha ya Josphe Nyuki akiwa nchini Kenya mdau wangu.
Kilicho nipelekea leo kukupa story nyingine ya Josphe Nyuki ni aina ya staili anayoitumia
kutangaza muziki wake Kenya.Ripota wangu www.unclejimmytemu.com aliyeko Kenya amekutana na Nyuki siku ya jana kwenye soko la nguo NAKURU KENYA akiwa na gari ndogo yenye spika juu na flat screen kubwa huku dereva wake anaweka muziki kisha Josphe Nyuki anashuka na kuanza kuimba akicheza kwa mbwembwe zake kaliiii.....huku akijitangaza yeye ni Mwinjilisti J.NYUKI.
Kwa mujibu wa ripota wangu ameifahamisha www.unclejimmytemu.com Nyuki hukusanya kundi kubwa la watu pindi anapoanza kucheza na hufanya hivyo kila kona la jiji la Kenya.
Hii ni picha aliyopigwa na ripota wangu,kulia ni gari yake.
Pamoja na ulemavu wa mkono mmoja Nyuki ni hatari kwenye jukwa.Picha hizi zilipigwa april 2,2013 na shekidele.
Hatariii!!
Nyuki akishambulia Jukwa.
0 comments: