i.Maisha baada ya kuzaliwa mpaka kifo
Japo
jamii nyingi huyatazama maisha ya mwanadamu katika hatua tatu: kuzaliwa, kuishi
na kufa na kimantiki inaweza kuonekana ni kweli lakini unapaswa kung’amua ya
kwamba kuzaliwa ni mlango wa kuingilia (entrance) na kifo ni mlango wa kutokea
(exit) kwenye jengo fulani. Katikati
ya hii miimo miwili ya kimaisha kuna wakati mkubwa wa maisha ambao ni vyema
tukaelekeza mioyo yetu ili tujipatie maarifa katika hilo.
Luka 2:40, 52
“Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa
hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.”
“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na
kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.”
Kupitia mistari hii unaweza kuona ya kwamba yule
mtoto alipozaliwa hakukua ndani ya siku moja na kufa hapo hapo, bali alipitia
hatua zote za ukuaji- naamini unaelewa ya kwamba ukuaji ni hatua, si mara moja
(growth is gradual not sudden). Kadiri alivyoendelea kukua ndivyo
alivyoukaribia mwisho wa maisha yake, lakini hakuwa anaishi kusubiri kifo. Kwa
namna ya kawaida utagundua kwamba alikuwa anaishi kama vile hakuna kifo mbele
yake, aliishi kwa kukamilisha kusudi la kuwepo kwake kabla ya kifo. Kitu
ninachotaka uone hapa ni kwamba kuna kiasi cha muda (time gap) kati ya kuzaliwa
na kufa au kwa maneno mengine kuna daraja linalounganisho hii miisho miwili ya
maisha. Wacha nikuonyeshe kwa maneno rahisi kabisa… ni kwamba, wewe hukufa mara
tu baada ya kuzaliwa (japo kuna matukio kama hayo) bali umeendelea kuishi mpaka
leo ukielekea kifoni. Hicho ndiyo kipindi ninachopenda tukitazame mahala hapa.
Yoeli
3:14
“Makutano
makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku
ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata maneno.”
Sote tunatambua wazi ya kwamba siku ya Bwana
haitakuja kwenye ulimwengu wa maisha ya kabla ya kuzaliwa kwetu na twajua ya
kwamba siku ya Bwana haitakuja kwenye ulimwengu ule wa maisha baada ya kifo.
Siku ya Bwana inakuja kwenye ulimwengu huu wa maisha ya katikati ya kuzaliwa na
kifo. Biblia inatufundisha ya kwamba Yesu hatakuja mara ya pili katika
ulimwengu wa maisha baada ya kifo, bali atakuja kwenye ulimwengu huu na hata
ndugu waliotangulia kuondoka kwa njia ya kifo na kuingia kwenye ulimwengu wa
maisha baada ya kifo, nao watarejeshwa ili kuungana nasi kwenye huu ulimwengu
(upande huu wa maisha) ndipo taratibu zingine zitafuata. (Ufunuo 1:7; 1
Thesalonike 4:13-17). Kwa lugha ya moja kwa moja ni kwamba bonde la kukata
maneno ni kipindi kati ya kuzaliwa mpaka kifo, ni hilo jengo fulani ambalo mtu huingia kwa kuzaliwa na huondoka kwa kifo,
yaani ni maisha mtu aishiyo baada ya kuzaliwa na kabla ya kufa. Ndugu msomaji,
naomba uanze kusoma fundisho hili kwa kujitambua kwamba umo ndani ya bonde la
kukata maneno!
0 comments: